NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala
Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemain Jaffo akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea banda la Global Education Link katika manesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam (DITF) maarufu kama Sabasaba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Education
link (GEL), Abdulmalik Mollel akifafanua jambo.
Wananchi waliotembelea banda hilo wakipata maelez ya huduma mbalimbali.
***********
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala
Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemain Jaffo amesema kuwa fursa za
elimu ni nyingi katika vyuo vya nje ya nchi na gharama zake ni nafuu.
Jaffo ameyasema hayo wakati wa
maonesho ya biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere
(Sabasaba) katika banda la Global Education Link (GEL),
amewataka Watanzania kutumia maonyesho ya Sabasaba kuwa ni kipindi
muafaka kupata mambo mengi kwa wakati mmoja likiwamo suala la elimu
katika vyuo vya nje.
Jaffo amesema kuwa, maonesho ya
sabasaba ni kipindi pekee kwa taasisi mbalimbali na huduma zake zinatolewa
bure.
Aidha amesema kuwa wazazi wanaotaka kuwasomesha watoto wao katika vyuo vya nje ya nchi kwa gharama nafuu watumie fursa hiyo kupita katika banda la Global Education Link (GEL) watapata taarifa mbalimbali.
Aliongeza kuwa kuna fursa nyingi
sio kwa serikali peke yake lakini hata kwa wazazi wenyewe kutumia fedha zao kwa
mambo ya msingi kuliko kufanya harusi ya Sh. milioni 50 au milioni
100.
Amesema sh.milioni 50 zinazotumika
katika harusi zinaweza kuziwekeza kwa vijana wetu katika kuwapatia elimu iliyo
bora zaidi kwa ajili ya uchumi wa nchi yetu tunaweza kufanya vizuri zaidi.
Jaffo amesema kuwa udahili wa
wanafunzi katika vyuo vya ndani katika uhandisi, Udaktari wa Binadamu ni
chache kutokana na mfumuko wa ufaulu kwa kidato cha sita pamoja na stashahada
hivyo wanaweza kusoma katika vyuo vya nje ambavyo vimeweza kuwekeza katika maeneo
hayo.
“Leo hii nikwambie ndugu
tembelea katika kila siku za mapumziko fanya tathmini kila harusi iliyopo
inayofanywa na sisi wenyewe ndio tunatengeneza harusi, unajikuta kumbe
tungekuwa na mpango mkakati mzuri wa kuhakikisha jinsi gani vijana wetu
tunakuwa na wataalamu katika sekta ya gesi, madini, kilimo pamoja
na viwanda vidogo vidogo kwani kwa miaka mitano wenzetu kutoka nchi mbali
mbali watakuja kutuchukua".amesema Jaffo.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Education
link (GEL), Abdulmalik Mollel amesema kuwa vijana wanaopitia kampuni yao hata
baada ya kupata udahili na kwenda masomoni nje ya nchi, wana utaratibu wa
kufuatiliwa maendeleo yao ili mzazi aweze kuona thamani ya fedha anayetoa kwa
kusomesha mtoto nje ya nchi.
Mollel amesema kuwa vyuo vya nje
wanavyokwenda wanafunzi kuna wawakilishi wanaofanya kazi moja kwa moja na GEL
ya kufatilia mienendo ya wanafunzi wao kwa kipindi chote wanachosoma na
taarifa zao zinatumwa na kisha mzazi kupewa taarifa za maendeleo ya mtoto.
Makamu wa Mkuu wa Chuo cha
Mzumbe, Profesa Lugano Kusiluka alisema kuwa GEL wanafanya kazi
vizuri katika kufanya utaratibu wa vijana kutafuta vyuo vya kusoma
ambavyo vinatambulika na TCU.
Amesema kuwa wanaona jinsi gani ya
kushirikiana na GEL na Chuo cha Mzumbe katika eneo la vyuo vya nje ili kuweza
kufika sehemu nzuri kwa kubadilishana uzoefu.
Anita Ituwe ,amesema kuwa wakati
alipokuwa anatafuta jinsi ya kupata vyuo vya nje walipata usumbufu lakini baada
ya kufika GEL walipata maelezo ya kutosha na kuweza kujiunga katika chuo kimoja
nchini India.
Nae Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa
Tanzania Taliki Abubakar ,amesema kwa wakati alipokuwa anatafuta chuo cha
kusoma alikuwa hana uhakika lakini baada ya kukutana na GEL aliweza kupata Chuo
cha kusoma na taratibu zilikwenda haraka.
No comments:
Post a Comment