July 25, 2016

BANCABC YAIWEZESHA BOT KUNUNUA NYUMBA ZA NHC MTWARA


Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akimkabidhi ufunguo
Gavana wa Benki kuu ya Tanzania- BOT Prof. Beno Nduru

Gavana wa Benki kuu ya Tanzania- BOT Prof. Beno Nduru akimsikiliza mkurugenzi wa masoko kitengo cha makampuni makubwa wa Bancabc Khilifa Zidadu wakati wa uzinduzi wa nyumba za BOT Mtwara na kushoto kwa gavana ni Mkurugenzi wa NHC Bw. Nehemia Mchechu.
Gavana wa Benki kuu ya Tanzania- BOT Prof. Beno Nduruakifafanua jambo kuhusina na ununuzi wa nyumba kwa ajili ya wafanyakazi wa benki hiyo mkoani mtwara, kulia kwa gavana ni mkurugenzi wa masoko kitengo cha makumpuni makubwa wa Bancabc Khalifa Zidadu na kushoto kwa gavana ni Mkurugenzi wa NHC Bw. Nehemia Mchechu. Gavana wa Benki kuu ya Tanzania- BOT Prof. Beno Nduru akibadilishana mawazo na mkurugenzi wa masoko kitengo cha makampuni makubwa wa Bancabc Khalifa Zidadu wa pili kushoto na Mkurugenzi wa NHC Bw. Nehemia Mchechu. aliyevaa fulana.
Mkurugenzi wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akitoa maelezo ya kukamilika kwa mradi wa nyumba kwa ajili ya wafanyakazi wa benki kuu ya tanzania mkoani mtwa kwa gavana wa benki hiyo prof beno nduru na mkurugenzi wa masoko kitengo cha makampuni makubwa wa Bancabc Khalifa Zidadu.
Gavana wa Benki kuu ya Tanzania- BOT Prof. Beno Nduru akimshukuru Mkurugenzi wa masoko kitengo cha makampuni makubwa wa Bancabc Khalifa Zidadu kwa kuwezesha BOT kununua nyumba hizo mkoani Mtwara, kushoto kwa gavana ni Mkurugenzi wa NHC Bw. Nehemia Mchechu.
**********
Shirika la nyumba la Taifa (NHC)limekabidhi nyumba za makazi kumi kwa banki kuu ya Tanzania(BOT) ikiwa ni sehemu ya nyumba walizozinunua katika mradi wa eneo la Shangani ambao katika utekelezaji wa ujenzi huo wameingia mkataba na Bancabc katika ununuzi wa nyumba hizo.

Mkurugenzi mkuu wa NHC,Nehemia Mchechu alisema hadi kukamilika kwa mradi huo utagharimu kiasi cha Sh 4.8 bilioni ambapo una majengo matatu yenye ghorofa tano kila moja ambapo kwa ghorofa zote zina nyumba za kuishi 30 zenye vyumba vitatu kila moja huku banki kuu wakiwa tayari wamenunua jengo mojalenye nyumba kumi.

“Nyumba hizi zinauzwa kwa wananchi, hadi hivi sasa benki kuu imenunua ghorofa moja yenye nyumba kumi za makazi ambapo kila moja ina vyumba vitatu vya kulala viwili vikijitegemea,jiko la kisasa lenye stoo,sebule ,sehemu ya chakula na stoo ya ziada na sehemu na kuogea na mita za maji na umeme,”alisema Mchechu

Aidha alisema shirika hilo lina mradi mwingine eneo la Raha Leo ambao pia wameingia mkataba na Bancabc ambayo imetoa fedha kwa ajili ya kufanikisha mradi huo ambao utagharimu kiasi cha 22.5 bilioni hadi kukamilika ambapo Benki kuu tayari imenunua majengo mawili yenye nyumba 40 kwaajili ya wafanyakazi watakaokuwa Mtwara.

Mkurugenzi wa masoko kitengo cha makampuni makubwa kutoka Bancabc,Khalifa Zidadu alisema NHC ni moja ya wateja wao ambao hushiriki kuwasapoti katika miradi yao ikiwa ni moja sehemu ya utendaji kazi wao.

“NHC ni moja ya wateja wetu ambao tumeshiriki katika kuwasapoti kwenye miradi miwili wa Shangani ambao tumewaunga mkono kwa asilimia 30 na mradi wa Raha Leo tumewapatia kiasi cha 11 bilioni ili kuufanikisha na hii ni sehemu ya utendaji kazi wetu,”alisema Zidadu

Aidha alisema benki hiyo kwa miaka miwili iliyopita wamekuwa wakishirikiana na makampuni makubwa na kuwaunga mkono na kuyataka makampuni na mashirika mengine kujitokeza ili kupata ushirikiano kutoka katika Benki hiyo.

“Niwaombe tu wananchi ambao wanahitaji kuwa sehemu ya miradi ya shirika la nyumba na miradi ya makampuni mengine watuone kwasababu tunaangalia pande zote na kuwaunga mkonoa,”alisema Zidadu

Akizungumza gavana wa benki kuu,Prof Benno Ndulu alisema ujenzi wa tawi la benki hiyo tayari umekamilika kwa asilimia 98 ambapo hadi kufikia mwezi Septemba wanatarajia watumishi waanze kuingia kwenye nyumba hizo na kuanza shughuli Novemba mwaka huu.

“Nyumba ni moja ya sekta zinazoongoza maendeleo,sisi tunataka kufungua milango ya shughuli zetu ifikapo Oktoba,nitoe rai hizi nyumba 40 zilizosalia zifanyike kila jitihada ifikapo mwezi Septemba mwishoni tuweze kukabidhiwa majengo yote mawili ili wale wanaotakiwa kufika huku wakute mazingira tayari waanze kazi,”alisema Prof Ndulu

Aidha alisema Tawi la Mtwara litakuwa likitoa huduma kwa serikali,mabenki,na shughuli mbalimbali za kiuchumi, katika kanda ya kusini na sehemu ya Pwani.

No comments:

Post a Comment