Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ineke Bussemaker akizungumza na Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru kabla ya kuanza kwa Mkutano Mkuu wa 16 wa mwaka wa benki hiyo uliofanyika, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika mkutano huo, wanahisa walibariki gawio la shilingi bilioni 52 lililotokana na faida ya shilingi Bilioni 150.2 ya faida baada ya kodi iliyoipata benki ya NMB ambapo Kila hisa itapata gawio la shilingi 104 kiwango ambacho ni cha juu kuliko benki yoyote nchini.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB Ineke Bussemaker,azkingumza na Mwenyekiti wa Bodi, Profesa Joseph Semboja wakati wa Mkutano wa 16 wa benki hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni kwa wiki.Katika mkutano huo, wanahisa walipitisha gawio la shilingi Bilioni 52 baada ya kupata faida baada ya kodi ya shilingi Bilioni 150.2 kwa mwaka 2015. Kwa gawio Hilo, Kila hisa itapata gawio la shilingi 104 kiwango ambacho ni cha huu kuliko benki yoyote nchini
Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ineke Bussemarker kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa 16 wa benki hiyo. kushoto ni Ofisa Mkuu wa Fedha wa NMB(chief finance officer), Waziri Barnabas. Mkurugenzi wa NMB alikuwa akitangaza maazimio ya wanahisa ambao walipitisha gawio la jumla la shilingi Bilioni 52 lililotokana na faida ya shilingi Bilioni 150.2 na hivyo Kila hisa ikipata gawio la shilingi 104 kiwango ambacho ni cha juu kabisa kuliko benki nyingine yoyote.
****************
BENKI ya NMB kwa mwaka jana imepata faida ya Sh. Bil. 150.2 kiwango ambacho ni kikubwa kuliko benki yoyote hapa nchini, faida hiyo ni zaidi ya asilimia 33 ya faida yam waka 2015 kwa benki zote.
Hayo yameelewa na Mkurugenzi wa NMB – Ineke Bussemaker katika Mkutano Mkuu wa 16 wa wanahisa wa benki hiyo uliofanyika jumamosi jijini Dar es Salaam, huku benki hiyo ikiainisha mafanikio makubwa kwa mwaka 2015 na maono ya mafanikio zaidi kwa mwaka 2016 matumaini ambayo wanahisa waliyapokea kwa mikono miwili.
Katika mkutano huo, wanahisa walipitisha gawio la shilingi Bilioni 52 ambapo kila hisa itapata gawio la shilingi 104. Kwa maana hiyo, serikali imepata gawio la shilingi Bilioni 16.5 kama gawio la hisa zake 31.8 wanazomiliki kwenye benki ya NMB.
Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas alisema "Tuna furaha kwamba benki imeendelea kuimarika kifedha katika kasi ile ile iliyopita, na nguvu ya ukuaji imezidi kuwa juu na kuongezeka kwa asilimia 18, hivyo kutanua thamani ya jumla ya taasisi hii, ikiwa ni pamoja na tahamni ya hisa zenu,"
Alifafanua ya kwamba, NMB imeendelea pia kutanua soko na pato katika mikopo na amana, na kwamba pato litokanalo na riba lilikua kwa asilimia 5 kutoka Sh. Bil. 417 mwaka 2014, hadi kufikia Sh. Bil. 438 kwa mwaka uliopita wa 2015.
"Licha ya faida ya jumla kuu kushuka kulinganisha na mwaka jana, lakini gawio la Wanahisa litabaki kama lilivyokuwa, ambako kila hisa moja itakuwa na thamani ya shilingi 104, uamuzi ambao ulifurahiwa na kupongezwa na wanahisa walioshiriki mkutano huo," alisema.
Alivitaja baadhi ya vikwazo vya maendeleo ya benki hiyo mwaka jana kuwa ni pamoja na mzunguko finyu wa pesa kutokana na harakati za Uchaguzi Mkuu, kushuka mara kwa mara kwa thamani ya shilingi katika soko la kubadilishia fedha.
Barnabas aliongeza kuwa, moja ya masuala muhimu ambayo NMB ilijikita kuyafanyia kazi mwaka jana ni pamoja na kumalizia uboreshaji matawi 98 waliyoachiwa na NBC ambayo yalikuwa katika hali mbaya na kuhamisha Makao Makuu ya Benki hiyo.
Aliongeza kuwa, katika kipindi cha miaka 10 sasa, NMB imejipambanua kama kinara miongoni mwa taasisi za kifedha, na kwamba moja ya ubinafsishaji ulioipa Serikali faida ni pamoja na wa benki hiyo.
0 comments:
Post a Comment