Meneja
Msaidizi wa TBL Mwanza,Gabriel Pitso,akiongea baada ya kupokea tuzo ya Mackay kutokana na kufanya uzalishaji kwa kutumia pumba za
mpunga.wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi
wa ufundi wa TBL Group, Gavin Van Wijk akiongea na waandishi wa habari na
wafanyakazi wa TBL Mwanza wakati wa hafla a kukabidhi tuzo
Meneja
Msaidizi wa TBL Mwanza,Gabriel Pitso,akipokea tuzo kutoka kwa Mkurugenzi wa
ufundi Gavin Van Wijk.
Baadhi ya
waandishi wa habari katika hafla hiyo.
Viongozi
wa kiwanda cha Mwanza katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kupokea tuzo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
**************
KIWANDA
cha TBL Mwanza kilichopo chini ya TBL Group na kikiwa moja ya kiwanda
kinachoshikilia rekodi ya ubora katika viwanda vya SABMiller duniani kimeshinda
tuzo kubwa ya Mackay kutokana na kufanya uzalishaji kwa kutumia pumba za
mpunga.
Mackay ni
tuzo kubwa ya SABMiller ya kumuenzi mmoja wa Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni
hiyo Graham Mackay ambaye katika kipindi chake cha kuitumikia kampuni hiyo aliendeleza
kwa kiasi kikubwa na alifariki miaka mitatu iliyopita ambapo kampuni imeanzisha
tuzo yake kwa viwanda vyake ambavyo vinafanya uzalishaji unaoendana sambamba na
malengo ya kampuni .
Malengo ya
SABMiller ambayo baadhi yake yanashahabiana na malengo ya Umoja wa Mataifa
yamelenga katika kufanya uzalishaji usio na athari kwa mazingira na unaoleta
mabadiliko kwa jamii kwa kuziwezesha kujikwamua kimapato.
Akiongea
baada ya kukabidhi tuzo hiyo kwa uongozi na wafanyakazi wa TBL
Mwanza,Mkurugenzi wa Ufundi wa TBL Group, Gavin Van Wijk,amekipongeza kiwanda
kwa kuendelea kungaa na kujinyakulia tuzo mbalimbali kama hii ya Mackay.
“Ushindani
ulikuwa mkubwa na ulihusisha viwanda mbalimbali lakini hatimaye
mmefanikiwa kunyakua tuzo hii na kuweka rekodi ya kuwa kiwanda cha kwanza
kuipata barani Afrika”.Alisema
Alitoa
shukrani kwa wateja wote wanaoendelea kuiunga mkono kampuni kwa kununua bidhaa
zake na kuongeza kuwa siku zote kampuni itahakikisha inaongeza uzalishaji
na kuingiza bidhaa bora sokoni ikiwemo kusaidia huduma mbalimbali zinazoleta
mabadiliko kwenye jamii.
Akiongea
juu ya tuzo hii katika hafla ya kuipokea iliyofanyika kiwandani Mwanza ,Meneja
wa kiwanda hicho Gabriel Pitso, alisema kuwa kiwanda hicho ndicho cha kwanza
kupata tuzo hii nchini na ushindi huu umetokana na kufanya uzalishaji
unaozingatia utunzaji wa mazingira kwa kutumia mashine zinazotumia pumba za
mpunga na mashudu ambao kitaalamu hujulikana kama Dry –De- Husking (DDH)
.
Alisema
kampuni mama ya SABMiller ilifanya utafiti na baada ya utafiti huo iliamua
kabla ya kuanzisha teknolojia ya uzalishaji usiotumia mafuta ya
dizeli kwenye viwanda vyake vyote ianzie katika kiwanda cha Mwanza ambapo
katika miaka ya kwanza ya majaribio mafanikio makubwa yamepatikana kutokana na
kutumia teknolojia hii ikiwemo kupunguza gharama za uendeshaji na kupunguza
uharibifu wa mazingira.
Mbali na
kupunguza athari za uharibifu wa mazingira na gharama za uendeshaji teknolojia
hii kwa kiasi kikubwa inasaidia kuongeza vipato kwa wakulima wa pamba na
mchele na wafanyabiashara wanaokusanya pumba kwa ajili ya kukiuzia
kiwanda .
“Zamani
pumba za mchele zilikuwa takataka lakini hivi sasa zimegeuka lulu kwa kuwa zina
soko tunazitumia katika uzalishaji hivyo kuna wafanyabiashara wanapita maeneo
mbalimbali wakizikusanya kwa ajili ya kutuuzia na huu ndio uwekezaji mzuri
unaonufaisha jamii inayoishi jirani na maeneo ya kiwanda na ni moja ya
malengo yetu”.Alisema.
0 comments:
Post a Comment