Mkuu wa Mkoa wa Lindi Akitoa Hotuba yake ya Ufunguzi ambapo Pia
Aliwataka Madiwani Kuacha Siasa katika Kutekeleza Maendeleo ya Halmashauri
zao,Kulia ni Mkurugenzi wa Shughuli za Mikoa Mradi wa Ps,Bw Conrad Mbuya
Baadhi ya madiwani na watendaji wa halmashauri za Kilwa na Ruangwa
Mkoani Lindi wakifuatilia jambo katika semina Elekezi ya Kujenga Uelewa kwa
Halmashauri kupitia Mradi kuimarisha Uwezo wa Kutoa Huduma kwa Jamii Chini ya Utekelezaji
wa Mradi wa PS3 Unaofadhiliwa na USAID
Afisa Mshauri wa Masuala ya Utawala Bora PS3, Nazar Sola akitoa Elimu
kwa Madiwani juu ya Utekelezaji wa Mifumo ya Utendaji na Utoaj. BOFYA HAPA PICHA ZAIDI
Joel Shimba,Mshauri wa Utawala Bora PS3(Kushoto )Wakielekezana jambo
na bw Victor Msoma,Mshauri wa Fedha PS3(Kulia)Kuhusiana na Mafunzo ya madiwani
wa Kilwa na Ruangwa Huku Bi Nseya Kipilyango,Mshauri wa Mifumo ya Tehama wa PS
3(Katikati)Akifuatilia kwa Umakini
Lukelo Mhenga Mhasibu Msaidizi(kushoto) pamoja na Fina Maziku wote wa
PS 3 wakifuatilia mada katika mafunzoa Hayo ambapo Halmashauri za Wilaya zao za
Kilwa na Ruangwa zikiwa ni Halmashauri za Awali kati ya 6 za Mkoa Huo
Zilizoanza utekelezaji wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya sekta za umma(PS3)
katika sekta za afya, elimu na kilimo.
Madiwani na Watendaji wa Halmashauri Pamoja na Wakurugenzi wa
Halmashauri Hizo ambao nao wanashiriki mafunzo hayo ya Siku 4
yanayofanyika Mjini Lindi
Madiwani na Watendaji wa Halmashauri Pamoja na Wakurugenzi wa
Halmashauri Hizo ambao nao wanashiriki mafunzo hayo ya Siku 4
yanayofanyika Mjini Lindi
********
Madiwani wa Halmashauri za Wilaya ya Kilwa na Ruangwa Mkoani
Lindi Zimeanza Utekelezaji wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma
(PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani
(USAID) kwa Kupatiwa Mafunzo ya Siku 4 na Kuratibiwa na Tamisemi
Kuanza kwa Hatua Hiyo kunafuatia kumalizika kwa Mafunzo kwa Watendaji
wa Halmshauri 6 Za Mkoa wa Lindi juu ya Namna ya Kushiriki na Kutekeleza Mradi
huo Utakaotekelezwa kwa Kipindi cha Miaka 5 Ijayo
Akifungua Mafunzo hayo,Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi amezitaka
Halmashauri Hizo Kufuatilia kwa Umakini Mafunzo yanayotolewa na wakufunzi wa
Chuo cha Mafunzo ya Serikali za Mitaa Hombolo ili Kupata Uelewa Juu ya
Uendeshaji wa Halmashauri.
"Madiwani ni kiungo muhimu baina ya serikali na watendaji wa serikali
madiwani Musipokuwa Vizuri Mtaburuzwa na Watendaji hususan katika Utendaji na
Utekelezaji wa Miradi hasa Ikiwa Diwani Una Tabia ya Kuomba omba na Kukopa kwa
Mkurugenzi au Mkuu wa Idara Lazima Mjipime Nyie Ndio wamiliki wa Halmashauri au
hamjijui?’’Alimalizia Zambi
0 comments:
Post a Comment