MKURUGENZI wa Mawasiliano wa Airtel
Tanzania, Beatrice Singano Mallya akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo
pichani) katika mkutano uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel
jijini Dar Es Salaam mwishoni mwa wiki hii akiongelea mafunzo mbalimali
yanayotolewa na “VSOMO” yaani VETA SOMO kufuatia uzinduzi wa mpango wa
Airtel wa kijamii ujulikano kama AIRTEL FURSA wakishirikiana na Mamlaka ya elimu ya ufundi Tanzania
(VETA) wiki moja iliyopita , ili kuwawezesha vijana kupata kozi mbalimbali
zinazotolewa katika vituo vya VETA nchini kupitia simu za mkononi
*************
VIJANA wa kitanzania wana kila sababu y a k u f u r a h i kufuatia
uzinduzi wa mpango wa Airtel wa kijamii ujulikano kama AIRTEL
FURSAikishirikiana na Mamlaka
ya elimu ya ufundi Tanzania (VETA) kwa kuanzisha application hiyo ya “VSOMO” yaani VETA SOMO
ulioanzishwa wiki moja iliyopita, ili kuwawezesha watanzania hasa vijana kupata
mafunzo mbalimbali yanayotolewa katika vituo vya VETA nchini kupitia simu za
mkononi . BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Lengo la VSOMO ni kuweza kusaidia
kupanua wigo wa mpango wa Airtel FURSA na kuwafikia vijana wengi zaidi hapa
nchini katika kutoa elimu kwa njia rahisi na nafuu kwa wote. Mpaka sasa kozi
zinazotolewa kutumia VSOMO ni ufundi pikipiki, ufundi umeme wa majumbani,
ufundi wa simu za mkononi , ufundi Alluminium, utaalamu wa masuala ya urembo na
ufudi wa kuchomea vyuma. Mafunzo haya yanapatikana kwa njia ya mtandao kwa wateja wote wa
Airtel wenye simu aina ya android
Akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za makao makuu ya Airtel
jiji Dar Es Salaam mwishoni mwa wiki hii, mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel,
Beatrice Singano Mallya, alisema “matumaini ya mpango huu unaolenga kutoa mafunzo kwa vijana ili waweze
kujifunza kutumia simu zao za mkononi na kuhitimu mafunzo ili kukuza biashara
zao na kupata taaluma zitakazowawezesha kujiajiri wao wenyewe na hata kutoa
ajira kwa vijana wengine.
Alisema kuwa mpango huu ambao unalengo la kufaidisha mamilioni ya
Watanzania hususan vijana na kuweza kujifunza masomo mbalimbali ili kuendelea
kuboresha kiwango cha elimu hapa nchini na kurahisisha upatikanaji wa elimu
sambamba na kuboresha utendaji wa kazi kwa vijana wetu,"
"Ninaomba watanzania kuitumia vyema nafasi hii ili kuboresha elimu
zao. Ninaamini kwamba kuanzia sasa watakuwa na muda mwingi wa kujisomea yote
hii ikiwa ni kutokana na kurahisishiwa kwa
kuweza kujisomea kupitia
VSOMO . Jinsi ya kujiunga ni rahisi sana, mteja atatakiwa kupakua VSOMO kwenye
orodha ya menu yake ya simu sehemu ya google play store na kujiandikisha
bure bila gharama zozote.
Mara baada ya kumaliza masomo
yake kwa 40% mwanafunzi atatakiwa kwenda kwenye kituo cha VETA kilichopo karibu
nae na kujiandikisha kwaajili ya mafunzo kwa vitendo ambayo yatachukua muda wa
wiki 2 kumaliza ikiwa ni sawa na masaa 60 na ndipo atakapokaa kwajili ya
mtihani na kutakiwa kufaulu kwa 60% “alisisitiza Mallya
Mallya alisema” Mwanafunzi atatahiniwa na kisha kuandikishwa na
kutakiwa kulipia kiasi cha ada yenye punguzo shilingi 120,000/= kwa kupitia
Airtel Money kwa kupiga *150*60#. Tunatoa wito kwa vijana kutumia fursa hii ya
kipekee ili kupata mafunzo ya ufundi kwa urahisi na gharama nafuu kwani gharama
ya masomo iko chini zaidi.”
0 comments:
Post a Comment