Mkurugenzi wa kampuni ya Darbrew Limited inayotengeneza Chibuku,David Cason akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Darbrew.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Darbrew wakifurahia tuzo hiyo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Darbrew Limited inayotengeneza Chibuku,David Cason akikabidhi tuzio hiyo kwa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Wafanyakazi wakiwa katika tafrija
Mkurugenzi wa kampuni ya Darbrew Limited inayotengeneza Chibuku,David Cason akijadiliana jambo na viongozi wa kampuni hiyo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Mkurugenzi wa kampuni ya Darbrew Limited inayotengeneza Chibuku,David Cason akiongea na wafanyakazi wakati ya hafla
ya kusherehekea kushinda tuzo ya uendelezaji vinywaji vya asili kutoka SABMiller iliyofanyika kiwandani hapo jana
******************
KAMPUNI ya Darbrew inayotengeneza pombe ya Chibuku
imetunukiwa tuzo kutoka SABMiller ya uendelezaji vinywaji vya asili nchini
katika kongamano la masoko la viwanda lililofanyika mjini Cape Town nchini Afrika ya Kusini.
Darbrew iliyopo chini ya TBL Group iliibuka kidedea baada ya
kushindanishwa na viwanda vinavyotengeneza vinywaji vya kienyeji vilivyopo
chini ya SABMiller vilivyopo katika nchi za Botswana,Malawi na Uganda.
Akitangaza mafanikio hayo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es
Salaam jana,Mkurugenzi Mkuu wa Darbrew, David Cason alisema kuwa tuzo hiyo ni
mafanikio makubwa kwa kampuni na aliwapongeza wafanyakazi wote kwa kujituma na
kuhakikisha yanapatikana mafanikio siku hadi siku.
“Tuzo hii sio ya mtu mmoja imepatikana kutokana na mchango wa kila
mfanyakazi wa DarBrew na inabidi kuongeza bidii zaidi katika kazi ili mafanikio
zaidi yapatikane na kampuni izidi kusonga mbele na kuwa miongoni mwa makampuni
makubwa ya vinywaji katika ukanda huu wa Afrika Mashariki”.Alisema Cason.
Alisema hatua ya kampuni kushindanishwa na viwanda vikubwa na kuibuka
na tuzo ni jambo la kujivunia kila mfanyakazi na aliwashukuru mawakala na wateja wote wa
Chibuku kwa kuunga mkono biashara ya kampuni.
Kwa upande wake Meneja wa Mauzo wa DarBrew,Freddy Kazindongo alisema
aliwapongeza wafanyakazi na kuwashukuru wateja kwa mafanikio yaliyopatikana na
kuongeza kuwa kampuni imejizatiti kuongeza zaidi ubora wa huduma za uzalishaji
na usambazaji na kuhakikisha kinywaji cha Chibuku kinawafikia wananchi popote
walipo na wanakipata kulingana na kila mtu na uwezo wake .
Katika kuthibitisha hilo alisema wiki hii kampuni imezindua chibuku
super ya mililita 750 ambayo itawawezesha wateja kupata kinywaji hicho kwa gharama nafuu.
Kazindogo alisema mkakati wa kampuni ni kuhakikisha urasimishaji wa pombe za kienyeji unafanikiwa
ambapo wananchi wataweza kupata kinywaji cha asili katika mazingira bora ya
usafi wakati huohuo wakikinunua wanachanga pato la serikali kwa njia ya kodi
kitu ambacho hakipo kwa pombe nyingine za asili.
Pia alisema kuwa kampuni itazidi kupanua wigo wa ajira za moja kwa moja
na zisizo za moja kwa moja ambazo zinawawezesha mawakala wakubwa na wadogo na akina mama wanaouza
pombe za asili kujipatia mapato ya uendesha maisha vilevile kupunguza uharibifu
wa mazingira kutokana na akina mama waliokuwa wanapika pombe za asili kwa
kutumia kuni na mkaa watakuwa wanauza pombe ambayo tayari imetengenezwa badala
ya kutumia muda mwingi kutengeneza pombe.
No comments:
Post a Comment