November 12, 2015

NGALAWA NDIYE MGOMBEA UBUNGE WA LUDEWA KUPITIA CCM



Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM iliyofanyika leo tarehe 12 Novemba, 2015 chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete imemteua Ndugu Deogratius Ngalawa kuwa mgombea wake wa Ubunge katika Jimbo la Ludewa mkoani Njombe.

Ndugu Ngalawa ameteuliwa kugombea nafasi hiyo ya Ubunge baada ya kushinda kura za maoni zilizofanyika Novemba 10, 2015.
 
Imetolewa na:-
 
Daniel Godfrey Chongolo,    
Kny: KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
12/11/2015

No comments:

Post a Comment