Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Profesa Jumanne Maghembe akizungumza
wakati wa kuzindua Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es
Saalam(Dawasa)jijini Arusha,katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Majisafi na Usafi wa Mazingirajiji la Arusha(Auwsa)Felix Mrema na Katibu
Mkuu wizara ya Maji,Mhandisi Mbogo Mfutakamba.
Katibu Mkuu wizara ya Maji,Mhandisi Mbogo Mfutakamba akizungumza wakati
wa kuzindua Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es
Saalam(Dawasa) jijini Arusha.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco,Mhandisi Cyprian
Luhemeja(kushoto)akijadilia jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Majisafi na
Usafi wa Mazingirajiji la Arusha(Auwsa)Felix Mrema(kulia) na Mkurugenzi
Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira,Mhandisi Ruth Koya
wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es
Saalam(Dawasa) jijini Arusha
*************
WAZIRI wa Maji,Profesa Jumanne
Maghembe amezindua Bodi mpya ya
Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam(Dawasa) na kuitaka kuhakikisha wanafanyakazi kwa bidii katika mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa ili kuondoa kero ya maji kwa wananchi.
Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam(Dawasa) na kuitaka kuhakikisha wanafanyakazi kwa bidii katika mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa ili kuondoa kero ya maji kwa wananchi.
Maghembe alitoa kauli hiyo jijini Arusha
na kusema kuwa serikali imepata kiasi cha dola za Marekani 409 kutoka Benki ya
Dunia,Korea Kusini na wadau wengine kuweka miundombinu ya majitaka
itakayosaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira kwenye bahari ya Hindi.
Alisema idadi ya watu katika jiji la Dar es
Salaam inaongezeka kila mara hiyo serikali imejipanga kuhakikisha inatengeneza
miundombinu itakayowezesha upatikanaji wa maji safi na maji taka unaondana na
hadhi ya jiji.
“Benki ya Dunia imetoa kiasi cha dola 220
milioni na Serikali ya Korea ya Kusini dola 89 milioni ambazo zitasaidia kwa
kiwango kikubwa kukabiliana na changamoto ya mahitaji ya maji na uboreshaji
miundombinu ya Maji taka,”alisema Profesa Maghembe
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji,Mhandisi Mbogo Mfutakamba alisema kumekua na maboresho
makubwa baada ya kuchimbwa visima virefu kwenye maeneo ya Kimbiji na Mpera hatua ambayo imewapa wananchi maji
kwa kiwango cha kuridhisha kufikia asilimia 68 ya mahitaji.
Mwenyeketi wa Bodi ya Wakurugenzi (Dawasa)Dk,
Eve Sinare alisema watashirikiana na
Menejimenti kukabiliana na changamoto za maji kwa kushirikiana Dawasco na
wadau wengine.
Alisema katika kipindi kilichopita bodi yake
ilipata mafanikio kutokana na kutokuingilia Menejimenti katika utendaji kazi
kwani sio jukumu la bodi kuingilia utendaji wa Dawasa wa siku kwa siku.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo ni Dk Eve Hawa Sinare,Makamu mwenyekiti wake ni Meja Jenerali Samueli Kitundu ambaye ni Mwenyekiti wa Dawasco huku wajumbe wengine ni Paul Sulley, Mhandisi Peter Chisawillo, Profesa Felix Mtalo,Lason Msongolena, Archard Mutalemwa, Abbas Mtemvu, Abdalah Bulembo,Mgeni Baruani na Dk James Wanyancha.
No comments:
Post a Comment