Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anaeungwa mkono na UKAWA, Edward Lowassa akipiga kura katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Nchini kote Oktoba 25, 2015. Lowassa alipigia kura Monduli, Mkoani Arusha.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli akipiga kura yake jimboni kwake Chato mapema leo asubuhi Oktoba 25, 2015.
Wakazi wa Bombambili,Kata ya Kivule wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye foleni ya kupiga kura katikavituo sita vilivyopo Shule ya Msingi Bombambili. Watanzania nchini kote hii leo wanapiga kura ya kuwachagua viongozi wao katika nafasi ya Urais, Wabunge, wawakilishi na Madiwani.
No comments:
Post a Comment