Mgeni Rasmi katika
Mahafali ya kwanza ya Shule ya Sekondari Adili High School,Moshono
Jijini Arusha,Profesa Raymond Mosha akiangalia kazi zilizoandaliwa na
wanafunzi wa masomo ya Sayansi ikiwa ni sehemu ya mahafali ya kidato cha
Nne.
Wazazi wa
wanafunzi wanaotarajia kuhitimu Kidato cha Nne wakifatilia kazi za
ubunifu zilizoandaliwa kwaajili ya kuonesha uwezo wao katika masomo ya
Sayansi kwenye Mahafali ya kwanza ya Shule ya Sekondari Adili High
School.
Wahitimu wakiwa na nyuso za tafakari kwenye mahafali ya kwanza ya Shule Adili High School iliyopo Moshono,Jijini Arusha.
Wanafunzi hao
wakionesha igizo linalopiga vita ukeketaji kutokana na madhara yake kwa
wanawake jambo linaloweza kusababisha ulemavu wa kudumu na vifo.
Profesa Raymond
Mosha akizungumza kwenye mahafali hayo,amesisitiza maadili kama msingi
mkuu wa mafanikio katika masomo na utendaji kazi,kushoto ni Mkuu wa
Shule hiyo,Mwalimu Andrew Shayo na Mwenyekiti wa bodi ya shule,Wakili
Modest Akida.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shule ya Sekondari Adili High School .
Mwanafunzi Nolam Mike akipokea cheti cha kuhitimu masomo yake kutoka kwa mgeni rasmi.
Wafanyakazi wakiburudika mbele ya wazazi na mgeni rasmi wakifurahia wahitimu wa kwanza wa kidato cha Nne.
0 comments:
Post a Comment