October 13, 2015

STARS VS ALGERIA NOVEMBA 14 TAIFA DAR ES SALAAM

Mchezo wa hatua ya pili kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwaka 2018 nchini Urusi kati ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Algeria (The Fox Desert) utafanyika tarehe 14 Novemba, 2015 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Taifa Stars itacheza mchezo huo dhidi ya Mbweha hao wa Jangwani siku ya Jumamosi Novemba 14, na mchezo wa marudiano kuchezwa siku tatu baadae Algeria 17 Novemba, 2015.

Kikosi cha Stars chini ya Kocha Mkuu Charles Mkwasa kimefanikiwa kusonga hatua ya pili ya michuano hiyo baada ya kuiondosha Malawi (The Flames) kwa jumla ya mabao 2-1, nyumbani ikishinda 2-0, na kufungwa 1 – 0 jijini Blantyre.

1 comment: