Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata
utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa jengo jipya la makao makuu ya NMB na
tawi jipya la NMB Private Banking kwenye jengo la makao makuu ya NMB
jana jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo ni Mwenyekiti wa bodi
ya Wakurugenzi wa NMB – Prof. Joseph Semboja(kushoto), Mkurugenzi Mkuu
wa NMB – Ineke Bussemaker (wapili kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam – Saidi Meck Sadiki (kulia) pamoja na wafanyakazi wa NMB.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Kikwete
akifurahia zawadi aliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa NMB – Ineke Bussemaker
(kushoto) jana katika hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la makao makuu
ya NMB na tawi jipya la wateja maalumu (NMB Private Banking) iliyopo
ndani ya jengo jipya la NMB.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania – Dr. Jakaya Kikwete
katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa NMB – Idara ya huduma kwa
wateja. Raisi Kikwete alikuwa anakagua Jengo jipya la NMB ambao ndimo
makao makuu mapya ya benki hiyo kubwa kuliko zote nchini.
Raisi
Jakaya Mrisho Kikwete amezindua rasmi jengo jipya na la kisasa kabisa
ambalo ni makao makuu mapya ya NMB lenye ghorofa saba huku likiwa na
uwezo wa kubeba wafanyakazi zaidi ya 800. Mbali na uzinduzi wa jengo
hilo, Raisi Kikwete pia alizindua tawi jipya la benki lililo ndani ya
jengo jipya la NMB.
Uzinduzi
wa jengo la makao makuu ya NMB ni mwendelezo wa maadhimisho ya Miaka 10
ya NMB ambayo yameadhimishwa kwa mafanikio makubwa. Baadhi ya mafanikio
ya benki hiyo ni pamoja na kukuza mtaji wake mpaka kuwa benki kubwa na
bora kuliko zote nchini huku ikiwekeza vya kutosha katika tekinolijia ya
mawasiliano inayowezesha benki kumudu kutoa huduma bora na karibu zaidi
ya wateja wake.
NMB
wakati inabinafsishwa mwaka 2005, ilikuwa na matawi chini ya 100, huku
ikiwa haina ATM hata moja na wateja si zaidi ya 600,000, hii leo
inapoadhimisha miaka 10 tangu kubinafsishwa, imefikisha matawi 173 na
ATM zaidi ya 600 huku ikifikisha wateja hai zaidi ya milioni mbili na
huduma zake zikienea mpaka vijijini.
Raisi
kikwete aliipongeza NMB na kusema kuwa serikali inajivunia benki hiyo
huku akiahidi kuwa serikali inaitunza benki kama mboni ya jicho na haina
mpango wa kuuza hisa zake. Serikali ina hisa asilimia 32.
No comments:
Post a Comment