Mgombea Ubunge Jimbo la Temeke kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Abbas Mtemvu, akizungumza na wananchi na wanachama wa chama hicho katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Keko eneo la Kachimbe Ubungo, Dar es Salaa jana.
Katibu Mwenezi wa Jimbo la Temeke, Ali Kamtande akihutubia jukwaani
Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo, Hassan Kitigi akizungumza na wananchi na wanachama hao
Wananchi na wanachama wakimsikiliza Mgombea Ubunge Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu
Mama mtemvu akisalimia wananchi na wanachama wakati wa Mkutano huo na kumuombea kura Mgombea nafani ya Urais ,Udiwani na kumuombea mumuwake
Sitti Mtemvu akiongea
Mgombea Ubunge kura za maoni CCM 2015, Arnold Mushi akizungumza na wananchi na wanachama wa chama hicho wakati wa mkutano uliofanyika katika Kata ya Keko eneo la Kachimbe Ubungo, Dar es Salaa jana .
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Temeke
kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abbas Mtemvu amesema amejipanga
vizuri kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo kwa miaka mitano mingine iwapo
atachaguliwa kushika nafasi hiyo.
Mtemvu alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika jana katika Kata ya Keko eneo la Kachimbe Umbungo jijini Dar es Salaam.
"Serikali na chama chetu cha CCM tuna
mipango ya maendeleo ya miaka mitano tuliyoindaa tunaomba mtuchague
tuweze kuikamalisha" alisema Mtemvu.
Alisema wakazi wa eneo hilo wasiwe na
wasiwasi wowote wala kuyumbishwa kwani kunafedha sh. bilioni 14 kwa ajili ya shughuli za maendeleo na uboreshaji wa
miundombinu .
Mtemvu alisema hivi sasa wamejiandaa
kujenga barabara za kiwango cha lami katika mitaa kadhaa ya Keko ambazo
zitawekwa taa za sola.
Aliongeza kwa kipindi ambacho
walikuwa katika uongozi wamefanikiwa kujenga miundombinu ya barabara,
kuweka taa na kujenga shule za sekondary mbili kati ya hizo zikiwa na
kidato cha tano na sita pamoja na kuhimarisha kwa huduma za afya kwa
kujenga zahanati jambo ambalo ni la kujivunia.
Mtemvu aliwaomba wananchi hao na makada
wa CCM katika nafasi ya urais wampe kura Dk. John Magufuli, Ubunge
wampe yeye na udiwani wampe Francis Mtawa ili mambo yaende sawa.
No comments:
Post a Comment