October 09, 2015

MGOMBEA UBUNGE WA CHAMA CHA ACT WAZALENDO ARUSHA MJINI ESTOMIH MALLAH AFARIKI DUNIA

Mgombea ubunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya ACT WAZALENDO Ndugu Estomih Malla amefariki dunia usiku wa leo saa saba katika hospitali ya KCMC Moshi.

Ndugu Malla alipelekwa KCMC jana mchana kutokea Hospitali ya St. Thomas iliyopo Arusha mjini baada ya kulazwa hapo kwa siku mbili kwa sababu ya kupata tatizo la shinikizo la juu la damu.

Hali hiyo ilimtokea siku ya tarehe 6/10/2015 mara baada ya kumalizika mkutano wa kampeni uliokuwa unafanyika Ngaramtoni,ambapo alilalamika kusikia kizunguzungu na baadae kukimbizwa hospital ya St Thomas ambapo madaktari wa pale walisema ndugu Malla anasumbuliwa na uchovu na hivyo anatakiwa kupumzika kwa muda mrefu. 

Sisi sote ni wa mola na hakika kwake sote tutarejea.

1 comment: