Unapozungumzia tasnia ya filamu nchini basi huwezi kuacha kuzungumzia makampuni ya kusambaza kazi za filamu Tanzania na Nje ya Tanzania. Kuna Makampuni mengi sana ambayo yanasambaza kazi za filamu ndani na Nje ya Tanzania lakini Katika Makampuni hayo huwezi kuacha Kuitaja Kampuni ijulikanayo kama PROIN PROMOTIONS LTD yenye makao yake Mikocheni na Mabibo.
Proin Promotions Ltd ni kampuni ya kutengeneza na kusambaza filamu za Kitanzania ndani na nje ya Tanzania ambapo Mwaka huu mwezi Agasti 30 ilitimiza Miaka mitatu tokea kuanzishwa Kwake na kuzinduliwa rasmi siku hiyo ya Agasti 31 2013 katika Ukumbi wa Mlimani City Unaweza kujiona HAPA jinsi uzinduzi ulivyokuwa huku siku hiyo ya Uzinduzi wa Kampuni hii ukienda Sambamba na Uzinduzi wa Filamu ya Msanii Elizabeth Michael almaarufu LULU iitwayo Foolish Age.
Ni Kampuni ambayo imeleta Ushindani katika Soko la filamu Tanzania haswa baada ya kuingia katika soko na kufanikiwa kuliteka soko la filamu kutokana na aina ya staili iliyoingia nayo kwenye soko la filamu. Ndani ya Mwaka mmoja Proin iliweza kutikisa katika soko la filamu kwa kuleta mabadiliko ambayo kiukweli yameweza kuonekana katika Tasnia hii ya Filamu nchini.
Kuingia sokoni na Staili ya kuuza Filamu iliyo na Sehemu Moja (Part 1tu) na Kutonunua hakimiliki za wasanii ni moja ya vigezo vilivyoipandisha Hadhi kampuni hii ya Kizalendo ambayo imelenga Kukuza na kunyanyua Tasnia ya Filamu nchini.
Leo hii unapozungumzia Swala la Filamu za Kitanzania hutoweza kuacha kutaja Kampuni ya Proin kutokana na Umahiri wake katika kutengeneza na kusambaza filamu na Ubora wa Kazi zake ambazo nyingi zimeweza Kuchukua tuzo Nchini Marekani huku Filamu yake Ya Kigodoro ikiwa mojawapo kati ya filamu nyingi za Proin zilizofanya Vizuri katika Soko la Filamu Nchini ukiachilia mbali Mapenzi ya Mungu, Family Curse, Never Give Up, Kutakapokucha, Mpango Mbaya, na ambayo imeingia Hivi karibuni Sokoni iitwayo Mwanaharusi Unapozungumzia Kantangaze" neno ambalo limechukua nafasi kubwa sana katika jamii ya Kitanzania sahivi basi hutoacha kuitaja Filamu ya "KIGODORO KANTANGAZE" ambayo ndipo neno hilo lilipotoka.
Proin Promotions imetoa takribani Filamu 25 tokea kuanzishwa kwake huku filamu zote zikiwa na viwango vya uhakika ambavyo zinaweza kuangaliwa na rika lolote lile huku ikijivunia Ubora wa Picha, Sauti na hata stori za filamu hizo.
Achilia mbali Kusambaza Filamu tu Proin Promotions ilikuja na Kitu ambacho mpaka leo kimeifanya Kampuni ya Proin Promotions Ltd kuwa juu kutokana na Uthubutu wake katika kuzunguka Mikoani kutafuta Vipaji vya vijana wenye uwezo wa kuigiza lakini hawakupata nafasi ya Kuonekana na mradi huo ujulikanao kama Tanzania Movie Talents (TMT)
Tanzania Movie Talents ni Shindano la Kuibua na kusaka Vipaji vya Kuigiza Nchini ambapo vipindi vyake vilikua vikirushwa kupitia Kituo cha Runinga cha ITV ambapo vijana wengi waliweza kupata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao huku washindi wa shindano hilo katika Mikoa walikua wakiondoka na Kitita cha Shilingi laki Tano huku mshindi wa Kwanza katika fainali hiyo akiibuka na Kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania. Shindano hilo kwa mara ya kwanza lilianza kufanyika Mwaka 2014 huku mshindi wa Kwanza katika fainali ya TMT 2014 iliyofanyika Mlimani City tarehe 30 Agasti 2014 kutoka Mtwara Mwanaafa Mwinzago Kuibuka Mshindi
Shindano la TMT limeweza kuleta mabadiliko katika tasnia ya filamu kutokana na kuzalisha vipaji na sura mpya katika tasnia ya filamu huku Ikiwa na Zao la Filamu Moja yenye viwango vya kimataifa iitwayo "Mpango Mbaya" Filamu hii ilitengenezwa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd huku ikichezwa na washiriki wa Shindano la TMT 2014 na kutoa nafasi kwa washiriki kujipatia kipato kutokana na utengenezaji wa filamu hiyo pamoja na mauzo ya filamu hiyo.
Proin Promotions Ltd Imeweza kuleta Changamoto katika tasnia ya filamu kutokana na kuzalisha vipaji na sura mpya katika tasnia hiyo huku washiriki wa TMT wakianza kuonekana katika baadhi ya Filamu za wasanii wengine kutokana na Kushiriki kwao katika filamu nyingine na baadhi ya Matangazo Lengo Moja wapo la Kampuni ya Proin Promotions Ltd limeweza kutimia na kuthibitika kutoka na kutoa nafasi kwa wasanii wachanga kuonekana na kuanza kufanya kazi ambapo zimeanza kuingia katika Soko la Filamu nchini.
Moja ya zao la Washiriki wa TMT ni filamu iitwayo Mpango Mbaya kama hujaweza kupata Nafasi ya Kuiangalia unaweza kununua nakala yako halisi na kujionea ubora wa kazi hiyo kuanzia Picha, Stori na Sauti. Vilevile wapenzi wa TMT wajiandae kukaa mkao wa kula kwa kupokea kazi nyingine mpya kutoka kwa washiriki wa TMT 2015 huku ikitarajiwa kuwa Ni nzuri zaidi ya washiriki wa Mwaka jana.
Kwa mantiki hiyo Kampuni ya Proin Promotions imeweza kuwa moja ya Kampuni mahiri katika Utengenezaji wa Filamu na Bidhaa za filamu nchini Tanzania.
Proin Promotions ltd iliweza kuhudhuria Maonyesho mbalimbali ya Kimataifa Nchini Kenya na kuweza kuliteka pia Soko la Filamu Nchini Kenya huku ikijipatia Mwanya wa kufanya kazi na wasanii wa Kenya. Na hii ndio Proin Promotions Ltd yenye Kumuongoza na Kumsimamia Kikazi Msanii Elizabeth Michael almaarufu Lulu.
Makala nyingine itakujia hivi karibuni
No comments:
Post a Comment