October 06, 2015

MAGUFULI AFANYA MKUTANO WA HADHARA JIJINI ARUSHA

????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeis jijini Arusha wakati akiwaomba wananchi wa jiji hilo kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika nchini kote na kushirikisha vyama mbalimbali vya kisiasa.

Amesema Mara atakapochaguliwa na kuongoza taifa la Tanzania serikali yake itamuenzi Wazriri Mkuu wa zamani kutoka jimbo la Monduli Mzee Edward Moringe Sokoine katika kupambana na Rushwa ambapo mzee huyo hakupenda kabisa watu ambao ni wala rushwa na wabadhirifu wa mali ya umma serikalini alipambana kufa na kupona ili kuwasaidia wananchi waliowanyonge.

Katika mkutano huo pia wanachama kadhaa waliokuwa viongozi wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo CHADEMA wamejiunga na chama cha Mapinduzi CCM na kutangaza rasmi katika mkutano huo, wanachama hao ni Japhet Sironga aliyekuwa Mwenyekiti Chadema wilaya ya Monduli na Jeremiah Mepukori Mwenyekiti BAVICHA wilaya ya Monduli ambapo wamekabidhi kadi zao kwa Dk. John Pombe Magufuli na kadi hizo kukabidhiwa kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia katika mkutano huo wa kampeni uliofanyika jijini Arusha leo.
????????????????????????????????????
Umati wa wananchi waliofurika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
????????????????????????????????????
Kattibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Arusha katika mkutano wa kampeni wa mgombea wa CCM Dk. John Pombe Magufuli. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

????????????????????????????????????
Kattibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Arusha katika mkutano wa kampeni wa mgombea wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Mjumbe wa kamati ya ushindi ya CCM Ndugu Christopher Ole Sendeka akimnadi Dk. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Ni Full Nyomi tu Aursha.
????????????????????????????????????
Msanii Ali Kiba akitumbuiza katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakiwa wamekaa meza kuu wakati mkutano huo ukiendelea jijini Arusha kutoka kulia ni Ndugu Christopher Ole Sendeka na Michael Lekule Laizer
????????????????????????????????????
Kindi la TOT likitumbuiza katika mkutano huo uliofanyika jijini Srusha.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakicheza muziki mara baada ya kuwasili kwenye mkutano katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakimsikiliza mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya kampeni CCM Ndugu Christopher Ole Sendeka.
????????????????????????????????????
Baadhi ya akina mama wa kimasai wakiwa katika mkutano wa kampeni mjini Monduli.
????????????????????????????????????
Magufuli hapa kazi tu.
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakiteta jambo walipkutana Longido.
????????????????????????????????????
Jeremiah Mepukori aliyekuwa Mwenyekiti BAVICHA wilaya ya Monduli akikabidhi kadi yake kwa Dk. John Pombe Magufuli huku Japhet Sironga aliyekuwa Mwenyekiti Chadema wilaya ya Monduli mwenye kofia akifurahia baada ya wote kujiunga na CCM jijini Arusha leo.
????????????????????????????????????
Arusha ni Magufuli tu leo.
????????????????????????????????????
Wasanii mbalimbali wakiimba wimbo maalum kwa ajili ya kampeni za Dk. John Pombe Magufuli uliozinduliwa leo jijini Arusha.
????????????????????????????????????
Wasanii wakiimba wimbo huo.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwana viongozi mbalimbali wakiwa katika jukwaa kuu kwenye mkutano huo jijini Arusha.
????????????????????????????????????
Yamoto Band wakafanya mambo makubwa sana Sheikh Amri Abeid.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Wabunge wanaogombea ubunge viti maalum mkoa wa Arusha CCM Viola Mfuko na Catherine Magige wakiwatunza vijana wa Yamoto Band wakati walipokuwa wakitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni wa CCM jijini Arusha.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa jiji la Arusha mara baada ya kuwahutubia kwenye mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
????????????????????????????????????

No comments:

Post a Comment