October 20, 2015

DKT FENELLA MUKANGARA AAHIDI KUIJENGA KIMBAMBA MPYA

Mgombea ubunge kwa tiketi ya ccm jimbo la kibamba dkt Fenella Mukangara
 Wananchi wakimsikiliza Mgombea ubunge kwa tiketi ya ccm jimbo la kibamba Dk Fenella Mukangara.
******
Na Jimmy Kagaruki,Kibamba
Mgombea ubunge kwa tiketi ya ccm jimbo la kibamba Dk Fenella Mukangara amesema atalifanya jimbo hilo kuwa la kisasa kwa muda wa miaka mitano ijayo.

Dkt Fenella ameyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni za ubunge jimbo la kibamba kwenye kata ya saranga.

Akihutubia mamia ya wananchi wa kata hiyo Dk Fenella amesema akichaguliwa katika kipindi cha miaka mitano atakabikiana na changamoto za kiuchumi ikiwemo ukosefu wa ajira, miundombinunha barabara, elimu na afya 

Kuhusu chanhamoto ya ajira dkt fenella amesema atahakikisha anazalisha ajira kwa vijana na akina mama kwa kuwaweka kwenye vikundi vya nguvu kazi iki wapate mitaji na iwe rahisi kwao kukopoesheka.

Ameonbeza musema kuwa atahakikisha anaanzisha mtandao wa mawasiliano jimboni humo ikiwemo kituo ca radio ya jamii ( kibamba fm ) ambacho kitakua kiunganishi madhubuti kwa wananchi wa jimbo la kibamba. " najua wananchi wa kibamba mna kiu na shauku ya kuwa na njia ya kuoaza sauti zenu, nawaahidi nitaanzisha radio yenu kibamba fm ambayo itatusaidia kisikuma maendeleo yetu mbele na hata kuzalosha ajira"


Dkt fenella amesisitiza wananchi wa jimbo hilo wasifanye makosa kiwachagua wapinzani bali wachague wagombea wote kutoka ccm ili wapate maendeleo ya kweli

No comments:

Post a Comment