Helokopta aina ya Eurocopter AS 350B3
yenye namba za usajili 5Y-DKK. Ilikuwa na uwezo wa kubeba tani 1.
HELKOPTA
iliyoanguka na kusababisha vifo vya watu wanne akiwepo Mgombea Ubunge wa jimbo
la Ludewa kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Deo Filikunjombe na rubani
wake, William Silaa ilikuwa mali ya Makamu wa Rais wa zamani wa Kenya, Kalonzo
Musyoka.
Kwa
Mujibu wa mtandao wa The Star wa Kenya, Helkopta hiyo AS 350B3 Eurocopter
yenye namba za usajili 5Y-DKK na iliyokuwa na namba ya uzalishaji 7027 na
ilikuwa imekodiwa na mgombea huyo wa CCM kwaajili ya kampeni zake jimboni Ludewa.
Mbali
na Filikunjombe pia watu wengine wa tatu waliotambulika kuwa ni Rubani wa
Helkopta hiyo, Capt. William Silaa, Kasablanka Haule na Egid Mkwela walifariki katika
ajali hiyo iliyotokea alhamisi jioni wakati ikitokea jijini Dar es Salaam
kwenda Njombe na kuanguka katika Msitu wa akiba wa Selous Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.
Helkopta
hiyo ilikuwa na uwezo wa kubeba mzigo
usiozidi tani moja na ikiruka urefu wa futi 20,000 kutoka ardhini.
Wachunguzi
wa ajali za ndege nchini Tanzania, wamechukua baadhi ya vitu kutoka katika
mabaki ya Chopa hiyo iliyoteketea kabisa kwaajili uchunguzi kubaini chanzo cha
ajali hiyo.
Helkopta
hiyo ni moja ya Helkopta nyingi zilizosajiliwa nchini Kenya, ambazo zimekudiwa
na wagombea mbalimbali wa Urais na Ubunge kwaajili ya kampeni za uchaguzi
zinazoendelea.
Kalonzo
alinunua helkopta hiyo ya kisasa kwaajili ya kampeni za uchaguzi Mkuu wa 2013
na imekuwa ikikodiwa ndani na nje ya Kenya kwa shughuli mbalimbali.
Kwa
mujibu wa mtandao wa www.aircraftcompare.com
Helkopta mpya AS350 B3 ina gharimu Shilingi bilioni 4.250 (dola Milioni 1.95)
bila gharama za kuinganisha.
Kenya
ina ndege binafsi takriban 400 zilizosajiliwa nchini humo ambazo zinamilikiwa
na watu binafsi wakiwamo, wakulima wakubwa, wafanyabisahara na wanasiasa
mashuhuri.
No comments:
Post a Comment