Kikosi cha wakongwe wa yanga kilicho wabugiza wakomngwe wenzao wa Simba 4-3.
TIMU ya Yanga veterani imeibuka mshindi wa mchezo wa
kirafiki dhidi ya Simba veterani ulioandaliwa na PSPF, Yanga iliibuka na
ushindi wa bao 4-3 na kubeba kombe. Mchezo huo ulifanyika tarehe 1 Januari 2015
katika uwanja wa chuo cha Bandari, Tandika jijini Dar es Salaam.
Hadi dakika tisini zinakamilika timu hizo zilitoka
sare ya bao moja kwa moja, mabao hayo yaifungwa na Omari kapilima kwa upande wa
Yanga na Barnabas Sekolo kwa upande wa Simba.
Bingwa wa mchezo huo alipatikana kwa njia ya matuta,
ambapo kwa upande wa Yanga walipata penalty ni Empram makoye, Ngada Shaganga,
Ismail Issa na Deo Lucas. Yanga ilikuwa ikifundishwa na Peter Tino Kasongo Athumani kwa Kwa upande wa simu waliozamisha penati ni Athumani
Chama, madaraka Selemani na Issa Manofu. Simba ilikuwa chini ya Kasongo
Athumani.
Lengo la mchezo lilikuwa kutoa burudani kwa wakazi wa
Jiji la Dar es Salaam na maeneo ya karibu hususani katika kipindi hiki cha sikukuu
za mwisho wa mwaka. PSPF itatumia fursa hiyo kutangaza huduma zake mpya ambazo
Mkopo wa Elimu na Mkopo wa Kuanza Maisha.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu
akisalimiana na wachezaji wa Yanga
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu
akisalimiana na wachezaji wa Simba
Mkurugenzi
Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu akizungumza na vyombo vya habari kabla ya mchezo
kuanza, kushoto ni Godfrey Ngonyani Mkurugenzi wa ukaguzi wa ndani
Simba wakipewa kombe lao
Mabingwa wakipewa kombe lao
Mabingwa wakiwa na kombe lao
Mchezaji wa Simba akijiunga na PSPF
No comments:
Post a Comment