Ridhiwani akihutubia wananchi katika Kitongoji cha Chalinze Mzee wakati wa ziara ya kuwashukuru wananchi na kusikiliza kero zao pamoja na kuwashuru kwa kumchagua, pia alisema atatumia unasheria wake kuwasaidia baadhi ya wakazi wa jimbo hilo wanaonyimwa haki zao za msingi ikiwemo kuporwa ardhi.
Mkazi wa Chalinze, Bibi akitoa malalamiko yake mbele ya Mbunge Ridhiwani Kikwete ya kudhulumiwa shamba lake na watu wasiojulikana.
Mkazi wa Chalinze Methodius Kaijage, akiuliza swali kuhusu alama za x zilizowekwa kwenye nyumba zao kwa ajili ya upanuzi wa barabara ambazo alidai ni takribani miaka kumi imepita bila kupewa fidia hivyo kusababisha kukosa maendeleo.
Sehemu ya wakazi wa Kata ya Bwilingu, wakiwa katika mkutano na mbunge wao mjini Chalinze.
Ridhiwani akimsalimia mmoja wa wazee wa Kitongozi cha Chalinze Mzee
Mmoja wa vijana wa Chalinze Mzee akiuliza swali
Mzee Ibrahim Koga akielezea mbele ya Mbunge asivyotendewa haki na Baraza la Kata ya Bwilingu la kuporwa ardhi yake
Mama mwenye Jamii ya Kimasai Rehema Lazaro akilalamika mbele ya mbunge kitendo cha baadhi ya wananchi kutoa lawama kwa wafugaji wote badala ya wafugaji wanaofanya vurugu kwa kupeleka mifugo kwenye mashamba ya wakulima na kuchafua visima vya maji.
No comments:
Post a Comment