January 07, 2015

MWIGULU AADHIMISHA SIKU YAKE YA KUZALIWA KWA KUTEMBELEA YATIMA, WAGONJWA NA KUCHANGIA DAMU

 Naibu Waziri wa Fedha,Mwigulu Mchemba leo ameadhimisha miaka 40 tangu kuzaliwa kwake. Katika maadhimisho hayo Naibu waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi ameitumia siku hiyo ya leo kwa kutembelea wagonjwa katika wodi ya Wazazi ya Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam, kuchangia damu pamoja na kuwatembelea na kuwapa zawadi yatima katika kituo cha CHAKUWAMA.
 Mwigulu akiwa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala.
 Mwigulu Mchemba akiangalia mmoja wa watoto waliozaliwa siku ya leo.
 Mwigulu Mchemba akitoa misaada ya vitu mbalimbali katika kituo cha yatima CHAKUWAMA.
Naibu Waziri Mwigulu Mchemba akichangia damu katika benki ya damu Salama.
Akipiga picha ya pamoja na watumishi wa Benki ya Damu Salama. Father Kidevu Blog inaungana na wananchi wa jimbo la Iramba Magharibu, Familia yake na watanzania wote kwa ujumla kumtakia heri na fanaka katika maisha yake na Mungu amjalie Hekima na Busara.

No comments:

Post a Comment