January 02, 2015

MASHALI DULLA HAKUNA MBABE

Na Michael Machellah.
MPAMBANO  wa ngumi za kirafiki kati ya Thomasi Mashali kutoka Manzese jijini Dar es Salaam na Abdalah Pazi kutoka Mwananyamala limetoka sare (Technical draw-dt) baada ya Thomas Mashali kuvuja damu nyingi toka juu ya jicho la kushoto alilopasuliwa kwa konde zito na mpinzani wake Abdala Pazi(Dullah Mbabe) mwishoni mwa raundi ya pili.

Raundi ya tatu mwanzoni Mashali alishambuliwa zaidi kiasi cha kukosa muelekeo ambapo pia damu zilizidi kutoka kushoto kwa jicho lake ndipo mwamuzi wa mpambano, Hakwe Mtulya alisimamisha mpambano kwa matibabu na baada ya Daktari kufanya uchunguzi wa kina ikadhihirika Mashali hawezi kuendelea na pambano hilo kwani damu zilikuwa zinatoka zaidi eneo la jeraha.

Kwa hatua hiyo mpambano ulikuwa ni droo kwa mujibu wa sharia za ngumi (Proffesional Boxing) kuwa mpambano unaoshia chini ya roundi ya nne ukiwa haujakamilika kwa ajali hiyo ni droo(Technical draw-dt).

Kabla ya matokeo hayo kutangazwa mashabiki wa ngome ya mashali walianzisha fujo iliyopelekea kuharibu viti,meza na watu kuumizwa ovyo ililazimika matokeo ktotangazwa na Katibu Mkuu wa Ngumi za kulipwa Tanzania(Tanzania Proffessional Boxing), Ibrahim Kamwe(Big Right) aliyathibitisha haya yote.

Mpambano wa Thomasi Mashali na Abdalah Pazi ulikuwa ni wa kirafiki wa  round inane(8), kutafuta kadi  unaowawezesha kugombania  Ubingwa ulifanyika juzi tarehe 1,1,2015 katika Ukumbi wa Manzese France Corner jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment