January 02, 2015

ABOOD ATOA MILION 11 KUTATUA KERO YA MAJI MKUNDI MOROGORO

 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akizindua Tawi la CCM la Wajasiriamali Bodaboda na Mama lishe lililopo Mgulu wa Ndege Kata Ya Mkundi Manispaa ya Morogoro.Mara Baada ya Kuzindua Tawi Hilo Mh Abood Aliongea na Wanachama wa Tawi Hilo Kisha Kuwaelekeza Kujiunga Kwenye Vikundi vya Wajasiriamali Yeye Atakuwa Tayari kuwawezesha Mitaji ya Kufanya Shuguli za Kujiletea Maendeleo.
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiwa Meza Kuu Sambamba na Katibu wa CCM Kata Ya Mkundi tayari Kusikiliza Kero zinazowakabili wakati wa Kata Hiyo Ambapo walimwambia Wanakabiliwa na Kero Kubwa ya Umeme,Maji na Barabara.Aidha Mh Abood Akitoa Majibu Kuhusu Kero Hizo Alesema Kuhusu Umeme Serikali Imeiweka Kata Hiyo Kwenye Bajeti ya Serikali ya Mwaka huu .Kuhusu Maji Mh Abood alitoa Shilingi Milioni 11 Kwajili ya Kununua Vifaa vya Kuwezesha Kufikisha Maji katika eneo la Mgulu wa Ndege Kata ya Mkundi.Pia Alitoa Shilingi Milion 2 kwajili ya Mafuta Ili Greda la Manispaa ya Morogoro Kuweza Kuchonga Barabarfa Zote za Kata Hiyo.
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Mgulu wa Ndege Kata ya Mkundi Jimbo la Morogoro Mjini Akisoma Risala yake Kwa Mbunge wa Jimbo Hilo Mh Aziz Abood. 
Mmoja wa Wakazi   wa Kata ya Mkundi waliojitokeza Kwa Wingi Kwenye Ziara ya Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Akieleza Kwa msisitizo Kero Kubwa Inayowakabili wakazi wa Kata Hiyo                   
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akiandika Baadhi ya Keo ambazo wananchi wa Kata ya Mkundi walimweleza wakati wa Ziara yake ya kutembelea Kata za Jimbo la Morogoro Mjini.
 Wakazi wa Kata ya Mkundi wakimsikiliza kwa Makini Mbunge wao
Wakazi wa Kata ya Mkundi wakimshangilia Mh Abood mara Baada ya Kutatua kero Kubw ya kata hiyo tatizo la Maji. 
  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akijibu Baadhi ya Kero zinazowakabili wakazi wa Kata ya Mkundi.

No comments:

Post a Comment