December 18, 2014

WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2015 HADHARANI

Naibu Waziri –Elimu Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI,Kassim Majaliwa (katikati) akizungumza na waandishi Dar es Salaam jana kuhusu wanafunzi waliochaguliwa kujiunga Kidato cha kwanza mwaka 2015.
Majina ya wanafunzi wa darasa la saba 2014 ambao wamefaulu na kuchaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari (kidato cha kwanza) mwaka 2015 yanapatikana katika mbao za matangazo katika shule za Msingi walizo soma watoto hao na katika ubao wa matangazo wa ofisi za Kata zilizo jirani. 



Hivyo wazazi na  wanafunzi wametakiwa kufika katika shule husika au katika Ofisi za Kata kuangalia majina ya wanafunzi hao na shule walizo chaguliwa. Pichani ni Baadhi uya wanafunzi na wazazi wakiangalia majina hayo katika ofisi ya Mtendaji Kata ya Makurumla jijini Dar es Salaam jana.

10 comments:

  1. Kwanini hawaja upload jamani wanatupa hard time

    ReplyDelete
  2. Ila katika shule ya msingi kigogo kuna majina 37 tu nayo yameandikwa kwa mkono yakiwa na yamegagawanywa hivi wasichana 25 na wavulana 12 sasa kwa kuwa kulikuwa na hizi sikukuu hakuna hata wakumuuliza sasa kwa kuwa nimepata mwelekeo kuwa na mengine yamebandikwa katika mbao za ofisi za kata ngoja nikaangalie maana majina mengi hayapo pale katika yaliyo bandikwa pale shuleni

    ReplyDelete
  3. kuna baadhi ya shule bado majina hayapo kama Shule ya Msingi Kigogo

    ReplyDelete
  4. majina ya shule yangewekwa kwenye mitandao ili iwe rahisi kwa wengine kupata
    had sasa hivi sijapata jina la shule alikopangiwa mwanangu!

    ReplyDelete
  5. tunaomba muweke majina ya shule kwenye mtandao kama mlivyoweka matokeo ya darasa la saba itaturahisishia sisi wengine kupata kwa urahisi.

    ReplyDelete
  6. Actuality our country in a case of full responsibility still so poor

    ReplyDelete
  7. Duh hata mimi nimehangaika sana kuyatafuta hayo majina na shule,wahusika jitahidini kwenda na wakati.

    ReplyDelete
  8. Dah yaani hard time kwel

    ReplyDelete
  9. Naomba mueke kwny mitandao mnatupa hardtime

    ReplyDelete
  10. please naomba muwekee majina online this is so bored cant you people understand we need to see them online please please

    ReplyDelete