WAZIRI wa Ardhi,
Nyumba na Makazi,Profesa Anna Tibaijuka amesema kuwa hawezi kujiuzulu katika
nafasi ya uwaziri kutokana fedha ya
Tegeta ESCROW.
Akizungumza na
Waandishi na Habari mapema leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Hoteli ya Hayyat
Regency, Profesa Tibaijuka alisema kuwa udalali wake wa fedha hiyo ni kwa ajili ya wanafunzi
katika shule za Taasisi ya Barbo Johansson Girls Education Trust, na kwamba fedha aliyoipata ni Bilioni Tshs. 1.66 ambazo zilitoka
katika kampuni ya James Rugemalira kama msaada kwa shule hiyo.
Alisema kuwa fedha hiyo kuingia katika akauti yake binafsi
ilitokana na masharti ya mtoa msaada ndugu James Rugemalira
ambaye alitaka fedha hiyo iingie katika akauti ya Benki ya Mkombozi.
"Nikijiuzulu hata Rais Jakaya Kikwete atanishangaa kwani fedha nilizopata ni za shule na kwa ajili kukomboa elimu nchini hasa kwa watoto wa kike kutokana na wazazi wengi kutoweza kumudu gharama za shule’’alisema.
Alisema kuwa udalali wake ni kutafuta fedha kwa ajili ya elimu nchini ambapo, alidai
hata Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt Reginald Mengi alitoa sh.milioni 248 kwa ajili ya msaada wa shule hiyo.
Profesa Tibaijuka alisema kuwa
wananchi watambue kuwa yeye ni mstaafu wa Umoja wa Mataifa hivyo hawezi
kufanya hivyo na kama angetaka fedha hiyo angeweza kufuata hata katika shule na
kuchukua.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Makazi,Profesa Anna Tibaijuka akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye hoteli ya Hyatt
Regency,Jijini Dar es salaam leo.
NA CHALILA KIBUDA WA MICHUZI MEDIA.
No comments:
Post a Comment