December 16, 2014

WAKAGUZI WA MIGODI WAPIGWA DARASA

Baadhi ya Wakaguzi wa Madini kutoka mikoa mbalimbali nchini, wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi (Kamishna Msaidizi wa Madini -Ukaguzi wa Migodi, Ally Samaje hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Wakaguzi wa Migodi kuandaa miongozo itakayosaidia katika  kutekeleza shughuli za ukaguzi wa migodi uliofanyika jijini Mwanza jana.

Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Idara ya Madini, Mhandisi Noel Baraka  akiongea jambo wakati akitoa mada kuhusu Ukaguzi wa Madini wakati wa kikao kazi cha Wakaguzi wa Migodi nchini.


Mtaalamu kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Mhandisi Chagwa Marwa, (kushoto) akichangia jambo wako wa majadiliano ya kuandaa checklist ya ukaguzi wa migodi. Anayesikiliza ni Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi, Assa Mwakilembe.



Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia ukaguzi wa Migodi (wa tatu kulia waliokaa ) katika picha ya pamoja na Wakaguzi wa Migodi  nchini waliohudhuria kikao kazi cha kuandaa checklist ya ukaguzi wa migodi.

No comments:

Post a Comment