December 12, 2014

VIJANA ELFU 10 WAMIMINIKA DIAMOND JUBILEE KUFANYA USAILI WA AJIRA ZA TRA LEO

Vijana takriban elfu kumi kutoka kila pembe ya nchi leo wamemiminika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam kusailiwa katika nafasi mbalimbali za ajira katika Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA). 

Vijana hao ambao wengi ni wale walio maliza vyuo mwaka huu na miaka ya hivi karibuni wamefika ukumbini hapo tangu saa kumi na mbili asubuhi na hadi muda wa saa 9:00 mchana bado walikuwa hawajaingia ndani kufanya usaili huo kutokana na wingi wa watu waliopo.

Usaili huo unasimamiwa na watumishi wa Chuo Kikuu cha Tumaini kampasi ya Mwenge jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wasailiwa wamelalamikia utaratibu unaotumika kwani ni wa mateso dhidi yao kwakua wanakalishwa kwa muda mrefu na baadhi kupoteza matumaini ya kufanya usaili huo. 

"Kiukweli hapa ni mateso, ndio tupo wengi tunaoatafuta ajira lakini kinachofanyika hapa ni kutesana na njaa na jua kali maana kila upande watu wamejaa na hata matumaini hadi sasa ya kufanya usaili huo ni mdogo," alisema mmoja wa vijana.
Hii ndio hali halisi iliyopo ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo vijana wengi wasaka ajira wamejazana hapo kusaka nafasi za ajira za TRA.

No comments:

Post a Comment