December 14, 2014

MREMBO ROLENE STRAUSS WA AFRIKA KUSINI TWAA TAJI LA MISS WORLD 2014

Malkia wa 64 wa Dunia amepatika usiku huu huko jijini London Uingereza ambapo Mnyange wa Afrika Kusini, Rolene Strauss amenyakua taji hilo na kuibuka Miss World 2014.

Nafasi ya pili na yatatu zimechukuliwa na Hungari pamoja na Marekani.

Hatua ya 11 bora ya shindano hilo waliingia warembo kutoka nchi za Australia, Mexico, Marekani,Kenya, Hungary, Brazil, Guyana, Uingereza , Afrikia Kusini, India na  Thailand .

Aidha awali katika hatua ya 25 bora waliingia warembo kutoka nchi za: Bolivia, Brazil, China, Jamhuri ya Dominican,Uingereza, Mexico, Guyana, Hungary, India, Indonesia, Malaysia, Afrika Kusini, Sudan Kusini, Vietnam,Finland, Ghana, Kenya, Netherlands, Philippines ,Australia, Russia, Scotland, Sweden, Trinadad and Tobago na Marekani.

 Mataji m,engine ni
Top Model: Bosnia & Herzegovina
Beach Fashion: Sweden
Multimedia: United States
Talent: Malaysia
Sports & Fitness: Finland
Beauty With A Purpose: India, Kenya, Brazil, Indonesia and Guyana

No comments:

Post a Comment