December 13, 2014

SIMBA YAIUA TENA YANGA 2-0 TAIFA HII LEO

Wachezaji wa Simba wakishangilia ushindi wa timu yao.
 Umati wa mashabiki wa Yanga.
 Umati wa mashabiki wa Simba.
Mashabiki wa Simba wakiwa wamebeba mfano wa jeneza kuwakejeli watani zao.
 Beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro'
HALI ya mji kwa upande wa soka la Tanzania leo itakuwa shwari baada ya Yanga kukubali kichapo cha goli 2-0 kutoka kwa hasimu wake mkubwa na mtani wake kisoka Simba.

Magoli ya Simbwa yalifungwa na Wachezaji Awathi Juma (dk 30) aliewahi mpira wa faulo uliopigwa na Mshambuliaji Emmanuel Okwi baada ya Kipa wa Yanga,Munishi Dida kuutema,Goli la pili lilifungwa na Elius Maguli (dk 41).
 
Matokeo haya ya leo huenda yakawa mwiba na tiketi kwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mbrazili Marcio Maximo kufuatia desturi ya Yanga ya kufukuza makocha pindi wafungwapo bna Simba katika mchezo wowote bila kujali kocha huyo kaifanyia nini Yanga.

Yanga iliwahi kufukuza kocha wake Ernie Brandts aliyeipa mafanikio makubwa timu hiyo na kuongpoza ligi lakini ilipofungwa na Simba tu 3-1 katika mchezo kam wa leo wa NANI MTANI JEMBE, Brandts alitupiwa virago nje.

Ushindi wa leo umeipa Simba heshima ya kuumiliki mji hadi hapo mwakani watani hao watakapo kutana tena katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania bara.

No comments:

Post a Comment