December 15, 2014

PSPF YATOA MKONO WA X MASS KWA VITUO VYA WATOTO WENYE UHITAJI MAALUM

 Kulia ni Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Mkoa wa Shinyanga Erick Chinimbaga na wa kwanza kushoto ni Afisa Fedha kutoka PSPF Makao Makuu Samweli Haule wakiwakabidhi zawadi za Krismasi watoto wenye ulemavu wa ngozi katika kituo cha Buhangija kilichopo Shinyanga  zawadi za Sikukuu ya Krismasi hapa watoto wenzao wakipokea zawadi hizo kwa niaba.  

Akikabidhi Msaada huo Afisa Fedha wa PSPF kutoka Makao Makuu alisema kwamba Mfuko wa Pensheni wa PSPF unalo lengo la kuwasaidia watoto wenye Uhitaji Maalum ili nao waweze kujisikia wapo katika jamii kama watoto wengine na kwamba kuwa hapo sio ndio kwamba wametengwa, alisisitiza kuwa Hata watakapo kuwa wakubwa wengine wataikuta PSPF na watakuwa wanachama na wengine watakuja kufanya kazi kabisa katika mfuko huo.
 Mlezi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima cha  Buloma Foundation kilichopo Picha ya Ndege Kibaha Bi Simphania Aidan wa kwanza kushoto akipokea Zawadi za Sikukuu ya Krismasi kwa niaba ya Msimamizi na Mwenye kituo hicho Bi.Fransisca Kyando Kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF , wa katikati ni Meneja wa PSPF Mkoa wa Pwani Msafiri Mugaka na wa kwanza kulia ni Afisa Mahusiano wa PSPF Coleta Mnyamani.  

Akikabidhi Msaada huo Meneja wa PSPF Mkoa wa Pwani Msafiri Mugaka alisema kuwa PSPF inatoa zawadi za Sikukuu ya Krismasi kwa watoto yatima ili nao washerekee vizuri na wasijisikie vibaya , aliongeza kuwa pamoja na PSPF kuwa na wanachama watu wazima lakini pia inafanya hivyo kwa watoto ili waanze kuijua PSPF wakiwa wadogo na wakiwa watu wazima waje kuikumbuka na kujiunga na Mfuko huo Bora wa Pensheni na hata kuja kufanya kazi katika Mfuko huo.

Nae Afisa Mahusiano wa PSPF kutoka Makao Makuu Coleta Mnyamani  Aliongeza neno kuwa Watoto yatima ni kama watoto wengine ambao wanahitaji kupata huduma na malezi Bora kama watoto wengine wenye wazazi au wanaolelewa bila shida yotote, alimalizia kwa kusema kuwa PSPF ipo pamoja na watoto hao wenye uhitaji na itaendelea kuwasaidia .
 Watoto wakipokea zawadi za Krismasi kwa Niaba ya wenzao
 Picha ya pamoja ya Ma Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF na watoto pamoja na Mlezi wao baada ya kupokea zawadi hizo kwa ajili ya Sikukuu ya Krismasi
 Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Mkoa wa Shinyanga wa pili kushoto  Erick Chinimbaga akimkabidhi zawadi Mmoja wa walezi wa watoto hao bwana Revocatus Robert   wa kwanza Kulia zawadi za Sikukuu ya Krismasi kwa Wasichana waliotoka katika Mazingira magumu wanaolelewa na Kituo cha Agape Mkoani shinyanga, wasichana hao walipata zawadi za Mafuta, Mbuzi, Mchele, Sabuni,Sukari pamoja na vitu.

No comments:

Post a Comment