MFUKO wa Pensheni wa PSPF umedhamini mchezo wa kirafki
utakaowakutanisha wachezaji waliowahi kuwika katika timu kongwe nchini Simba na
Yanga.
Mchezo huo unatarajiwa kufanyika tarehe 1 Januari 2015 katika uwanja wa chuo cha Bandari, Tandika jijini
Dar es Salaam, kiingilio kitakuwa
bure ikiwa ni zawadi ya mwaka mpya kutoka PSPF.
Katika mchezo huo baadhi ya wachezaji wa Simba wanaotarajiwa
kushuka uwanjani ni Thomas Kipese, George Lucas, Bita John, George Masatu,
Mustafa Hoza, Emmanuel Gabriel, Idd seleman. Timu ya Simba inafanya mazoezi
katika uwanja wa Leaders uliopo
Kinondoni, ipo chini kocha mchezaji Kasongo Athuman.
Wanaotarajiwa kushuka uwanjani kwa upande wa Yanga ni Peter Manyika, Mwanamtwa Kihwelo, Edibily
Lunyamila, Mohamed Husein, Chibe Chibindu, Aboukar Salum, Bakari malima. Yanga
wanafanya mazoezi katika uwanja wa kauda ulipo katika makao makuu ya klabu hiyo
kariakoo Jijini Dar es Salaam, wakiongozwa na kocha Peter Tino.
Lengo la mchezo huo ni kutoa burudani kwa wakazi wa
Jiji la Dar es Salaam na maeneo ya karibu hususani katika kipindi hiki cha sikukuu
za mwisho wa mwaka. PSPF itatumia fursa hiyo kutangaza huduma zake mpya ambazo
Mkopo wa Elimu na Mkopo wa Kuanza Maisha.
Tunatoa mwito kwa wapenzi wa soka
kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo ili kuwaona wakongwe waliowahi kutikisha
nchi katika anga ya soko nchini.
No comments:
Post a Comment