December 23, 2014

MACHINGA WA KARIAKOO WAFUNGA BARABARA, POLISI WAWATAWANYA KWA MABOMU NA RISASI

Moto ukiwaka katika barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam jirani na mataa ya Kamata kufuatia vurugu zilizotokana na Machinga wa Kariakoo kuzua tafrani baada ya mgambo wa jiji kukamata mali zao.

Father Kidevu Blog, alishuhudia magari kadhaa ya Polisi wa kuzuia ghasia (FFU) yakiwasilia katika eneo hilo na kufanikiwa kuwatanya Machinga hao na kurejesha hali ya amani katika eneo hilo ambapo kutokana na vurugu hizo njia zilifungwa na magari kushindwa kupita kutokana na mawe yaliyokuwa yamewekwa njiani.
 
Mkazi wa Dar es Salaam akikimbia kuvuka eneo hilo la Kamata.
 Polisi wa kiendelea kuondoa watu katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment