Kaimu
Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule (kushoto),
akimkabidhi, Ofisa Elimu wa Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Kibaha, Doris
Semkiwa (kulia), bati na rangi zenye thamani ya sh.milioni 3.5
zilizotolewa na mfuko huo jana, kusaidia ujenzi wa maabara katika Shule
ya Sekondari ya Mihande ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Jakaya
Kikwete za kuhakikisha kila shule ya sekondari nchini inakuwa na
maabara. Anayeshuhudia makabidhiano hayo katikati ni Mkuu wa shule hiyo,
Flora Masha.
Kaimu
Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule (kushoto),
akipeana mkono na Mkuu wa shule hiyo, Flora Masha wakati akikabidhi
msaada huo. Kulia ni Ofisa Elimu wa Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Kibaha, Doris Semkiwa.
Kaimu Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule (kushoto), akipeana mkono na Ofisa Elimu wa Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Kibaha, Doris Semkiwa. Kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Flora Masha.
No comments:
Post a Comment