Akiwa ana nyimbo za
“Mwana” na “Kimasomaso” zikiongoza katika vituo mbali mbali Africa,
Alikiba aachia video ya “Mwana” iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu jana
,Ijumaa tarehe 19 Decemba 2014 kwa mamilioni ya mashabiki Africa na
duniani. “Mwana” ni nyimbo ya kwanza baada ya kufunga mkataba wake na
kampuni ya Rockstar4000 Management na Rockstar Publishing.
Rekodi
ya “Mwana” ni nyimbo ya kwanza kutoka kwenye albamu ya tatu ya Alikiba
baada ya kutokuwa katika muziki kwa muda wa miaka mitatu. Alikiba
alifafanua kwa kusema “ Hii ni album itayoonyesha kukua kwangu kimuziki
na kuonyesha utofauti mbali mbali katika kipaji changu nilichojaliwa.”
Alikiba
alitoa kibali ili video ya “Mwana” iruke hewani jana “exclusively” kwa
masaa 24 kwenye vituo vya televisheni vitano Africa katika vipindi
maarufu kwenye vituo hivyo na kuwafikia mashabiki zaidi ya milioni 500
kwa pamoja.
Vituo vya televisheni hivyo ni Clouds TV kuonyesha exclusive Tanzania, Nation TV kuonyesha exclusive Uganda, One Music Networks kuonyesha exclusive Cameroon, Angola, Ethiopia, USA na UK, Sound City kuonyesha exclusive Nigeria na Ghana na Citizen TV exclusive kwa upande wa Kenya, DRC Congo na Rwanda
No comments:
Post a Comment