July 16, 2014

MMOJA AFA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA KUANGUKIWA NA LORI LA KOKOTO MOROGORO LEO JIONI

Majira kama saa 11.30 eneo la bene msavu barabara ya iringa lori kubwa lilokuwa limebeba kokoto liliacha njia na kupinduka na kuwaangukia wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza fulana cha Mazava ambao wengi wao ni wasichana mpaka sasa mtu mmoja amefariki na majerui wengine wamepelekwa katika hospitali ya mkoa wa morogoro na hali zao si nzuri. Kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Leonald Paul amethibitisha tukio hilo Eneo ilipotokea ajali hiyo ilikuwa vilio,uongozi wa kiwanda haujazungumza chochote. Father Kidevu Blog itawajuza zaidi.

No comments:

Post a Comment