January 11, 2014

ZIARA YA NAIBU KATIBU MKUU WA HABARI, VIJANA NA MICHEZO MKOA WA PWANI

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Bi.Mwanamvua Mrindoko akimweleza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel(mwenyeshati Jeusi) Mpango wa kuendelea kuwawezesha vijana katika halmashauri yake kwa Kutekeleza mipango mbalimbali iliyowekwa ikiwamo kutoa mafunzo kwa vijana na kuongeza bajeti hadi kufikia shilingi milioni 40 kutoka milioni 10 iliyokuwa inatolewa hapo awali kwa mwaka wa fedha 2014-2015,wakati wa Ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo kuangalia shuguhuli mbalimbali za vijana zinazoratibiwa na Wilaya hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel(mwenyeshati Jeusi) akiongea na vijana wa kikundi cha bodaboda wakati wakati wa Ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo kuangalia shuguhli mbalimbali za vijana leo katika wilaya ya Kisarawe.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel(mwenye suti  Jeusi) akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa kikundi cha bodaboda kutoka katika wilaya ya Kisarawe, wakati wa ziara yake ya kuangalia shuguhuli mbalimbali za vijana zinazoratibiwa na Wilaya hiyo
Afisa Maendeleo ya Jamii ya Vijana Toka Wilaya ya Mkuranga Bi.Safina Msemo akimweleza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel(kushoto) Mafanikio yaliyotokana na Utoaji wa asilimia tano(5%) katika pato la halmashauri kwa ajili ya shughuli za vijana,pia uandaaji  wa kambi ya vijana ya siku 40 watakayoshirikiana na Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) kwa ajili ya kutoa mafunzo mbalimbali hasa katika sekta ya ujenzi, wakati wa Ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mkoani Pwani.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel akimsisitiza Afisa Maendeleo ya Jamii ya Vijana Toka Wilaya ya Mkuranga Bi.Safina Msemo(kulia) kuendelea kusimamia na kuratibu shughuli zinazotekelezwa na vijana katika Wilaya hiyo ili kuweza kuwasaidia kuleta maendeleo kwa Vijana
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel akisaini kitabu cha wageni alipotembelea kikundi cha MWAMKO FARM GROUP katika wilaya ya Mkuranga.kulia kwake ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga Bi. Joyce Nampesya na Mbele yake ni Mwenyekiti wa Kikundi hicho Bw.Hemed Kassim.
Wanakikundi cha MWAMKO FARM GROUP toka Wilaya ya Mkuranga eneo la Kimanzichana wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel wakati wa ziara yake Mkoani Pwani.
Sehemu ya Miradi wa Kikundi cha MWAMKO FARM GROUP toka Wilaya ya Mkuranga,mbali na Ufyatuaji wa Matofali pia wanajishughulisha na ulimaji wa Miti ya miembe na uuzaji wa maji kwa wanakijiji wa eneo hilo kutokana na Visima viwili wanavyovimiliki.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na wanakikundi cha MWAMKO FARM GROUP na baadhi ya Maafisa toka Wilaya ya Mkuraga.
Mwanakikundi cha NAMPULA CARVINGS Bw.Steven Mwidumbi akimuonesha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel(mwenye suti NYEUSI) kinyago mfano wa nyani wanaodandia Miti,wakati alipowatembelea leo katika wilaya ya Mkuranga.(Picha zote na Hassan Silayo-MAELEZO)

No comments:

Post a Comment