Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akizungumza wakati wa maadalizi ya ufungaji wa mafunzo ya vijana wawakilishi wa vikundi kutoka mikoa mbalimbali kuhusu utengenezaji wa matofali ya ya udongo yenye teknolojia ya Interlocking Blocks yaliyoanza Januari 6 mpaka 17 mwaka huu ambayo yanatarajiwa kufungwa wiki ijayo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda, Mkurugenzi huyo amesema Shirika la nyumba badala ya kwenda kutoa msaada wa sabuni na vyakula katika vituo vya watoto yatima au kusaidia biskuti limeamua kubadilisha maisha ya vijana wa Tanzania kwa kuwapa mafunzo na kuwapatia mashine za kutengeneza matofali ya udongo ambayo wao NHC watakuwa ndiyo wateja wakuu wa kununa matofali hayo, lakini pia shirika hilo linatoa mashine za kufyatulia matofali zipatazo 640 katika wilaya 160 mikoa yote ya Tanzania bara na kiasi cha shilingi 500,000 kila mkoa kama mtaji wa kununulia saruji kwa vikundi hivyo, Katikati ni Injinia Kwanama Elias Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo kutoka Nation Housing&Building Research Agency (NHBRA) na kushoto ni Bw.Julius Njelwa kutoka VETA, mafunzo hayo yameratibiwa kwa pamoja na (NHC), (VETA) na (NHBRA) kwa pamoja. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akizungumza akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari leo.
Injinia Kwanama Elias Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo kutoka Nation Housing&Building Research Agency (NHBRA) akifafanua masuala ya kitaalamu kuhusu teknolojia hiyo ya matofali kwa waandishi wa habari.
Baadhi ya maofisa wa Shirika la Nyumba NHC wakiwa katika maadalizi hayo kushoto ni Suzan Omary Meneja Mawasiliano NHC, Muungano Saguya Meneja huduma kwa jamii NHC na Ephraim Kibonde mtangazaji wa Clouds Radio.
No comments:
Post a Comment