Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akikata utepe kuzindua shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki,
wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar leo Jan
10, 2014. Kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ali Juma
Shamhuna.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akifunua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la Msingi la shule ya
Sekondari ya Kiembe Samaki, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa shule
hiyo iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar leo Jan 10, 2014.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Kiembe Samaki, wakitoa burudani wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akizungumza na mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya
Kiembe Samaki, baada ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo uliofanyika leo Jan 10, 2014, mjini Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akizungumza jambo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kiembe
Samaki, Amina Salum Khalfan, wakati alipokuwa akitembelea chumba cha
Maabara baada ya kuzindua rasmi Shule hiyo wakati wa hafla fupi
iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar leo Jan 10, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akikagua moja ya vitabu vya kumbukumbu za Maktaba ya Shule mpya
ya Sekondari ya Kiembe Samaki wakati alipotembelea chumba hicho cha
Maktaba baada ya kuzindua rasmi Shule hiyo wakati wa hafla fupi
iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar leo Jan 10, 2014. Kulia ni
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Amina Salum Khalfan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari
ya Kiembe Samaki, Amina Salum Khalfan, wakati alipotembelea katika
chumba cha Mawasiliano na mafunzo ya Kompyuta cha shule hiyo, baada ya
uzinduzi rasmi wa shule hiyo uliofanyika leo Jan 10, 2014, mjini
Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akitembelea chumba cha Maabala kati ya vyumba vinne vilivyopo
shuleni hapo.
No comments:
Post a Comment