January 24, 2014

Ligi kuu ya Vodacom – Mzunguko wa pili kupitia AzamTV pekee



Ligikuuya Vodacom sasa itarushwa moja kwa moja kupitia Azam TV ili washabiki wa mpira wa miguu Tanzania waweze kujionea mechi kali  za ligi kuu muda wowote na mahali popote zitakapochezwa. Ligi hizi zitaonyeshwa katikati na mwisho wa wiki.
Ratibazamwishowa wiki hii:

Jumamosi tarehe 25 Januari:
Ashanti United na Young Africans zitacheza Uwanja wa Taifa (DSM)
Azam FC na Mtibwa Sugar zitacheza Uwanja wa Azam Chamanzi (DSM)

Jumapili tarehe 26 Januari:
JKT Ruvu na Mgambo JKT zitacheza Uwanja wa Azam Chamanzi (DSM)
Simba SC na Rhino Ranger zitacheza Uwanja waTaifa(DSM)
Ratibaza wiki ijayo:
Jumatanotarehe 29 Januari:
Azam FC na Rhino Rangers JKT zitacheza Uwanja wa Azam Chamanzi (DSM)
Coastal Union na Young Africans zitacheza Uwanja wa Mkwakwani (Tanga)

AlhamisTarehe 30 Januari:
Ruvu Shooting na Mbeya City zitacheza Uwanja wa Mabatini (PWANI)

Mechi zitaonyeshwa moja kwa moja kuanzia saa kumi kamili jioni.
Katika habari nyingine mpya na zakusisimua,  mashabiki sasa watakuwa na uwezowakuangalia dondoo za mechi zote kupitia simu za mkononi, ikiwapa fursa ya kuangalia matukio yaliyopita na kujua yatakoyojiri mechizijazo. 

“Baada ya kupata kibali cha kuonyesha ligi kuu ya Vodacom, moja kati ya malengo makuu ni kuhakikisha kuwa tunafikia kiwango cha juu cha kimataifa. Katika kufanikisha hili, tumewekeza Zaidi  kwenye teknolojia yakisasa ya matangazo ya nje na mafunzo ya wafanyakazi wetu. 

Na  tumedhihirisha hilo kwamba tumejizatiti katika kutoa matangazo yenye ubora wa hali juu tulipo rusha Ligi ya kombe la Mapinduzi lililomalizika hivi karibuni”  Amesema Rhys Torrington, mkurugenzi mkuu wa Azam Media.

Azam Media Ltd waliingia mkataba wamia kamitatu (3) na TFF wa haki za kutangaza na kuonyesha mechi zote za ligi kuu ya Vodacom wenye thamani ya Tshs 5,560,800,000.

Azam TV tayari inaonyesha chaneli Zaidi ya 50, zinazojumuisha chaneli maarufu za kimataifa na za kitaifa na chaneli tatu maalumu kutoka Azam. Chaneli hizo maalumni:

Azam One – Burudani motomoto kwako na familia kutoka bara la Afrika, ambazo nyingi ni kwalugha ya Kiswahili.

Azam Two – Programu maalum mbalimbali zilizo chaguliwa ulimwenguni.
Sinema Zetu – Chaneli maalumu inayoonyesha filamu za kitanzania masaa 24.

Kwa ujumla, chaneli hizi zinawapa fursa wateja wetu kuweza kuangalia kiwango cha juu cha michezo mbalimbali, filamu, vipindi vya watoto, tamthilia, maisha na burudani na mengineyo kwa beinafuukabisayaTshs 12,500/= tu!

Kwa sasa Azam TV inapatakana Tanzania tu, lakini kwa wiki chache zijazo itaanza kupatikana Uganda na Kenya, kabla ya kuenea Afrika Mashariki kwa ujumla. 

Kwa ujumla AzamTV inakupa nafasi ya wewe na familia ya kukupa ta burudan imbalimbali kwa bei rahisi nanafuu.

Azam Media itaendelea kuwekeza kwenye utengenezaji wa programu mpya za ndani ya nchi kupitia kampuni tanzu ya Uhai Productions kwa ushirikiano na watengeneza vipindi wa kitaifa.

No comments:

Post a Comment