MKUU wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma,
Christopher Kangoye, amesema vijana wakiwezeshwa kikalimifu kushiriki shughuli
za uzalishaji, umasikini Tanzania utakuwa historia.
Pia, amewaasa vijana kutumia elimu walizonazo
katika kujiajiri ili kuharakisha maendeleo badala ya kukaa vijiweni na kubaki
kuwa walalamishi na wakati mwingine kutumiwa na wanasiasa kama ngazi ya
kutimiza malengo yao.
Kangoye, ambaye amekuwa mhamasisha mkubwa wa
vijana nchini, amesema Tanzania inaweza kuwa taifa linalotoa misaada kwa nchi
zingine na kuachana na utegemezi iwapo vijana wataitambua na kutumika
kikamilifu kwa shughuli za maendeleo.
Aliyasema hayo juzi wakati alipokuwa
akizungumza na vijana katika sherehe za kusimikwa Kamanda wa UVCCM wilaya na
makamanda wa Kata wilayani Kongwa, ambapo Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai, alisimikwa
kuwa Kamanda wa Vijana wilaya.
Kangoye, ambaye alikuwa mgeni rasmi, aliema Hayati
Baba wa Taifa, Julius Nyerere na Nelson Mandela ni alama ya harakati za vijana
katika maendeleo na ukombozi wa Bara la Afrika na kwamba, walianzisha mageuzi
hayo wakiwa vijana.
‘Vijana wanatakiwa kuwa mstari wa mbele
kukataa umasikini kuanzia ngazi ya familia hadi taifa kwwa kufanya kazi kwa bidii
ili kuleta mageuzi ya kiuchumi katikka taifa letu. Tanzania inaweza kuwa taifa
linalotoa misaada badala ya kuwa tegemezi iwapo vijana watajitambua na kuitoa
kuleta maendeleo.
‘Muda wa kukaa vijiweni na kuilalamikia
serikali haupo, tuna fursa na rasilimali nyingi zinazoweza kuleta mageuzi ya
kiuchumi na kutufanya kuwa taifa tajiri,’ alisema Kangoye.
Alisema harakati zozote ziwe na kisiasa,
kiuchumi na kijamii huanzia kwwa vijana na kwamba, ni wakati sasa wa kuamka na
kuleta mageuzi kwa maslahi na ustawi wa Tanzania ya sasa na inayokuja.
Naye Ndugai akizungumza baada ya kusimikwwa
kuwa Kamanda wa Vijana wilayani humo, aliungana na Kangoye kwa kuwataka vijana
kujituma katika shughuli za uzalishaji ili kuacha kuwa tegemezi.
Alisema kuna vijana wengi wenye elimu na
ujuzi wa kutosha, lakini hawataki kufanya kazi na badala yake wanasubiri serikali
iwafanyie kila kitu, jambo ambalo amesema haliwezekani.
‘Tufanye kazi ndugu zangu ili tuachane na
umasikini na kuwa tegemezi, fursa zipo za kutosha kinachotakiwa ni kuamua kama
alivyosema DC Kangoye ili tulete mageuzi kwenye taifa letu’ alisema.
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Kongwa, Asia
Alamga, alisema kabla ya kuwasimika makamanda hao walifanya shughuli mbalimbali
za kijamii ikiwa ni pamoja na kutembelea wafungwa, wagonjwa kwenye hospitali za
wilaya na kata na kutoa misaada ya kijamii.
No comments:
Post a Comment