December 21, 2013

WADAU MBALIMBALI WALA NONDO CHUO KIKUU MZUMBE TAWI LA DAR ES SALAAM JANA

 Karani wa fedha wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Leah Amani (kulia) ambaye amehitimu Shahada ya Uzamili katika Sayansi (Uhasibu na Fedha) akipongezana na mhitimu mwenzake wa Shahada ya Uzamili katika Utawala wa Umma, ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Angela Kiziga wakati wa mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu Mzumbe tawi la Dar es Salaam jana.
Baadhi ya wahitimu wakiwa bize na simu zao jana kabla ya kuanza kwa mahafali hayo.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Joseph Kuzilwa (wa pili kulia) akiwa pamoja na Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho, Prof. Josephat Itika (wa pili kushoto) na Kaimu Mkuu wa Chuo, Prof. Daniel Mkude (kulia) wakati wa mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi ya Dar es Salaam jana.  Kushoto ni Bw. Ludovick Utoh ambaye ni Rais wa Baraza la wahitimu Chuo Kikuu Mzumbe.
Baadhi ya wahitimu katika mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi ya Dar es Salaam jana.  Katika mahafali hayo, jumla ya wahitimu 1225 walipata shahada za uzamili katika makundi nane ya programu mbalimbali.
IMG-20131221-WA000 
Margareth Simalenga, akipozi kwa picha mara baada ya kuhitimu shahada ya uzamili katika Uongozi wa biashara (usimamizi wa mashirika) yaani Master in Business Administration (Corporate Management) katika mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu cha Mzumbe Cumpas ya Dar es salaam yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment