Wekundu wa Msimbazi simba ya jijini Dar es Salaam leo imefanikiwa kwa mara nyinge kuzima kidomo domo, mikogo na mbwe mbwe za kila namna za watani wao wa jadi Yanga kwa kuwafunga magoli 3-1 katika mchezo maalum wa NANI MTANI JEMBE mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hii leo.
katika mchezo huo Magoli ya simba yaliwekwa kimiani na mshambuliaji wake mahiri mwenye kasi nyingi na mbinu lukuki za ufungaji Hamisi Tambwe ambaye alipachika magoli 2 huku bao la tatu likifungwa na mchezaji aliyesajiliwa dirisha dogo kutoka Mtibwa Awazi Juma huku goli la Yanga likifungwa na Emmanuel Okwi.
Patashika ya kuwania mpira
Hali jukwaa la yanga ilikuwa si shwari sana...
Ngome hata iwaje ndio Simba walipita...
Simba wao ilikuwa shangwe tu...
No comments:
Post a Comment