December 03, 2013

MWENYEKITI CHADEMA SINGIDA AJIUZULU



                                                            WILFRED NOEL KITUNDU
MWENYEKITI CHADEMA MKOA SINGIDA
S.L.P 260
3.12.2013

KATIBU WA CHADEMA MKOA
S.L.P 260
SINGIDA
YAH: - KUJIUZURU UENYEKITI MKOA SINGIDA
Somo hapo lahusika,
Ninapenda kukuarifu kuwa nimeamua kujiuuzuru nafasi yangu ya uenyekiti wa mkoa ambayo nimekuwa nikiitumikia kwa kipindi kirefu sasa kama kielelezo cha kuamini na kudai demokrasia ya kweli ndani ya chama.

Ikumbukwe kwamba mimi ndio mwanachama wa kwanza kujiunga na CHADEMA mkoa wa SINGIDA na ni mwanachama wa 300 kitaifa, hiyo ni heshima kubwa sana kwangu na sipo tayari kuipoteza kwa kukubali kuwa sehemu ya udharirishaji huu wa demokrasia uliopitiliza

Maamuzi na vitendo vinavyoendelea ndani ya chama chetu kwa sasa ni ubakaji na udharirishaji wa demokrasia ya kweli tunayoihubiri mbele ya umma.

Kwa barua hii basi, nimeonelea bora upate ufahamu huo kuwa si vema mimi kuendelea kupingana na dhamira yangu inayonituma kuwa mwanademokrasia wa kweli.

Kwa kipindi hiki kifupi mnaweza mkaendelea kuitumia anuani yangu ya posta mpaka hapo mtakapopata anuani yenu tayari.

Ninatanguliza shukrani zangu za dhati kwa wanachadema wote wanaopinga upuuzi huu uliofanywa na kamati kuu ya chama.

Kusimamia haki, katiba na misingi ya chama ni wajibu wangu, hivyo kwa namna yoyote ile sitaweza kuwa tayari kufumba macho pindi ujinga wa namna hii unapoendelea kutekelezwa kwa uwoga wa uchaguzi.


Nakutakia kila la heri kwenye majukumu yako.

………………………………………………….
Wilfred N. Kitundu






MSIMAMO WA MWENYEKITI CHADEMA MKOA WA SINGIDA DHIDI YA UAMUZI WA KAMATI KUU YA CHAMA

  
UTANGULIZI
Ikumbukwe kwamba mimi ndio mwanachama wa kwanza kujiunga na CHADEMA mkoa wa SINGIDA na ni mtu wa  300 kitaifa kujiunga na Chama hiki. Nimejiunga mwaka 1992 siku ya mkutano mkuu kwanza wa uzinduzi chama uliofanyika mnazi mmoja.

Nimekuwa nikijitolea vya kutosha nguvu, muda na akili zangu nyingi kukijenga na kukilinda chama hiki mpaka sasa mkoa wetu wa singida umepata wabunge watatu mmoja wa kuchaguliwa na wawili wa viti maalum.

Tangu mwaka 1992 mpaka 2011, chadema imekuwa ikitumia nyumba yangu kama ofisi, nimekuwa nikifanya hivyo kama kielelezo change cha kudai na kupigania demokrasia ya kweli ndani ya nchi kwa kuijenga CHADEMA imara.

Kwa kipindi chote hicho nimekubali kujibana na kuipunja familia yangu stahili zake ili chama chetu kikue kwa kasi mkoani kwetu, nashukuru mungu wanasingida waliitikia ombi nletu na kutufuta majozi yaliyotokana na jasho langu kwa kutupatia mbunge mwaka 2010.

Hivyo nimehudhunika sana kwa kitendo kilichofanywa na wajumbe wa kamati kuu cha kukiuka utaratibu na kujivalisha mamlaka yasiyowahusu.


HISTORIA YA USALITI KWENYE CHADEMA
Viongozi wa chama chetu wamekuwa na historian a tabia ya kutubadilishia wasaliti na kuwapachika kila aina ya shutuma kila kunapokaribia uchaguzi ndani ya chama.

Tuliambiwa na kuaminishwa kuwa KABURU ni msaliti mkubwa ndani ya chama.

Tukaambiwa na kuaminishwa kuwa CHACHA WANGWE alikuwa msaliti, tukafanyishwa vikao vya ndani, tukaanzishiwa mikakati mbali mbali kuwa wangwe ni msaliti na kwamba anatumika.

WANGWE alipofariki hali ikatulia kidogo, tukaanza kuimba na kumsifia kwamba ni kamanda, tukamuita majina yote ya kishujaa lakini haikuwa na faida yoyote.

Sasa hivi tumeanza kuaminishwa wasaliti wengine wapya, safari hii wasaliti hawa wamevuka usaliti na kuwa WAHAINI, masikitiko yangu ni hawa wahaini ndio wale wale wengine waliokuwa wakikitetea chama kipindi kinapingwa na waliokuwa wasaliti.
Bahati mbaya sana na cha kufurahisha kama si cha kusikitisha hakujawahi kutokea Msaliti, Mhaini Wala kiongozi yeyote anayetuhumiwa kukihujumu chama mwenye asili ya KILIMANJARO ama KASKAZINI kwa ujumla, wahaini na wasaliti wote wanatokea mikoa yetu sisi wanyonge.

WAVAMIZI NDANI YA CHAMA

Bahati mbaya sana, harakati hizi za kuibua na kuwashuhulikia hawa wanaoitwa wasaliti zinafanywa na wavamizi ama wahamiaji ndani ya chama, nitatoa mifano michache muda huu.

1.       GODBLESS LEMA tulimpokea kwenye chama hiki mwaka 2009 akitokea TLP aliposhindwa kufanya siasa za ushindani baada ya kushiriki kukiua chama hicho, lema alikwenda TLP akitokea NCCR-mageuzi aliposhindwa kutimiza malengo yake ya kisiasa na kushuhudia akikiua chama hicho. Leo LEMA ndio mpambanaji mkuu dhidi ya Zitto Kabwe, Dokta Kitila mkumbo na demokrasia ya kweli ndani ya chama chetu, anaambatana na kijana mwengine anaitwa MAWAZO, huyu wakati sisi tunapambana na CCM mwaka 2010 kuwanadi wagombea wetu wa ubunge urais na udiwani, yeye alikuwa anagombea udiwani kupitia CCM tuliyokuwa tunaipinga, ameingia chadema na sasa wale waliokuwa wanampinga akiwa huko leo anawaita WASALITI na WAHAINI.

2.      MCH. MSIGWA naye huyu ni hivyo hivyo tulimpokea CHADEMA baada ya kushindwa na kuigombanisha NCCR na baadae TLP. Baada ya kuvimaliza vyama hivyo sasa wamehamia chadema kutugombanisha na kutuharibia chama chetu kwa makusudi kabisa.

3.      Wengine vinara kwenye mgogoro huu ni Tundu Lissu, bensoni kigaila, john mrema na wengineo hawa ni vijana tuliowapokea kuja kujenga chama na sio kukibomoa chama kama wanavyofanya

4.      TUNDU LISSU yeye ni kinara sana wa kumshambulia zitto kwenye hili, lakini ninasikitika kusema kuwa Tangu nimekuwa mwanachadema na Tangu nimemfahamu Lissu alipohamia CHADEMA hajawahi kufanya mkutano hata mmoja wa kujenga chama ndani ya mkoa wa SINGIDA ukiondoa jimboni kwake. Tumemuona Zitto akitoka bungeni na mara nyingine hata kigoma kuja kufanya mikitunano maeneo mbali mbali hapa singida ikiwemo iramba, singida mjini na kwingineko, na mtakumbuka zitto amewahi kukamatwa na polisi mkoni singida akikinadi chama, hakuwa lissu. Sasa leo anapotoka mbele na kujinadi kuwa ana mapenzi mazuri na chama kushinda zitto kabwe ni upuuzi unaopaswa kukemewa kwa nguvu kubwa sana.

Ninasikitika sana kuona Mwenyekiti Mbowe na Katibu mkuu Slaa wanawakumbatia hawa, ninashangaa sana kuona viongozi hawa wanakubali kuwa sehemu ya ubakaji huu mkubwa wa demokrasia.

Ninaamini kabisa vijana hawa wanatumiwa na mwenyekiti na katibu mkuu kuutumia uzoefu wao walioutumia kwenye vyama vyao vya awali mpaka kuviua.


KUHUSU KAMATI KUU NA MAAMUZI YAKE.

Uamuzi wa kuwavua nyadhifa zitto kabwe na wenzake kwa madai ya kuwa na mkakati wa siri wa uchaguzi, ni uamuzi wa kipuuzi na wa kupuuzwa, kwenye hili kamati kuu imedhihirisha namna gani inaundwa na watu wasio na weledi na hawaongozwi na misingi na taratibu za chama.

Katika chama chochote kile, kamati kuu haiwezi kuwa mshitaki mkuu, hiyo hiyo iwe mwendesha mashitaka, hiyo hiyo iwe shahidi, hiyo hiyo iwe hakiku na hiyo hiyo iwe muandika hukumu. Hapa wamedhihirisha ni namna gani wanaongozwa na Hisia na chuki zinazotawaliwa na hofu ya uchaguzi ndani ya chama.

Kamati kuu hii ya sasa haipo kwa ajili ya maslahi ya wanachama na chama kwa ujumla, ipo kwa maslahi ya mbowe na slaa pengine na watu wa kaskazini.

Kwa hiyo kuwazuia watu wenye mawazo tofauti na wao na kuwaita wasaliti na wahaini ni sawa kuasisi na kuimiza mpasuko ndani ya chama, maana kuna mambo kamati kuu inaweza kufanya na kuna mengine haiwezi, hii haiwezi kufanya hili walilolifanya sasa hawawezi kulifanya.

Nionavyo mimi na wanachama ninaowaongoza hapa singida ni kwamba kamati kuu imekurupuka na kufanya maamuzi yaliyotawaliwa na hofu, chuki na uroho wa madaraka dhidi ya zitto kabwe na wenzake walioonyesha nia thabiti ya kukivusha chama kwenye harakati za kuilikomboa Taifa.

MSIMAMO WA CHAMA  SINGIDA

(i)                 Tunalaani, kuipinga na kuikemea kamati kuu ya chama dhidi ya maamuzi yao haya ya kipuuzi yaliyojaa chuki, hofu na wasiwasi mwingi kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani ya chama

(ii)               Tunamtaka mwenyekiti na katibu mkuu waitishe mara moja mkutano wa baraza kuu la chama kutolea maamuzi suala hilo.


(iii)             Tunamtaka katibu mkuu awazuie wakurugenzi na maafisa wake aliowatuma kusambaa mikoani kusambaza waraka wa siri unaowachafua zitto na kitila na kwamba kufanya hivyo ni kujidharirisha wao wenyewe.

(iv)             Tunampa onyo kali katibu mkuu Dkt. Slaa kuwa asithubutu kukanyaga SINGIDA ikiwa bado hajayafanyia kazi maelekezo yetiu hapo juu, kuzunguka kwake mikoani baada ya kumvua vyeo zitto ni kwenda kuthibitisha kuwa amefanya makusudi mpango wake huo.


(v)               Tunapenda wanachadema na watanzania watambue kuwa Hatuna Imani na Mwenyekiti wa Taifa wa chama, Katibu Mkuu wa Chama, Kamati kuu kwa ujumla na tunamuagiza mbowe aivunje mara moja kisha nay eye ajiudhuru.



MWISHO

Kutokutii maamizio yetu haya ni kusababisha mgogoro usiokuwa na kikomo ndani ya chama hiki,

Singida tunasema kuwa ‘’ kamati kuu inaweza kumvua zitto kabwe uongozi, inaweza kumuondolea heshima yake ndani ya jamii, inaweza pia kumsingizia kila aina ya uwongo itakavyo, lakini kamwe kamati kuu haiwezi KUZUIA MPASUKO NDANI YA CHADEMA.’’




Kwa kuzingatia utangulizi wangu hapo mwanzo, na kwa kuona ukweli kwamba chama chetu sasa kimevamiwa na kuwa na vyama viwili ndani ya chama kimoja,

Nimeonelea ni vyema sasa niilinde na kuithibitisha dhamira yangu ya demokrasia ya kweli, nimeona ni vema nihakikishe demokrasia tunayoiimba tunaitenda kwa vitendo.

Kwa misingi hiyo sasa, nimeamua kukaa pembeni ya udhalimu huu wa demokrasia unaoasisiwa na viongozi wakuu wa chama wanaoogopa kivuli cha uchaguzi mkuu wa ndani ya chama,

Nimeona ni vema sasa niuthibitishie umma wa Tanzania kuwa kwenye chadema unaruhusiwa kugombea vyeo na nafasi zote isipokuwa uenyekiti wa Taifa ndio maana zitto tuliyemuunga mkono leo hii anashambuliwa kwa dhamira yake safi ya kidemokrasia.

Nimechoka sasa, nimebadili mawazo, sipo tayari tena kuwa msukule wa fikra mbele ya watu wanaopenda kuigiza na kujifanya watetezi wa wanyonge kumbe ni wanafiki wa kutupwa.

Nimememuandikia barua katibu wangu wa mkoa kumueleza maamuzi yangu ya kujiudhuru uenyekiti wa mkoa, sihitaji tena kuwa mwenyekiti wa mkoa kwenye chama ambacho hakitendi kinachoyasema, sihitaji tena kuwa mwenyekiti wa mkoa kwenye chama ambacho dakika na saa yoyote unaweza ukageuzwa na ukaitwa msaliti na muhaini wa aina ya kopekee.

Mimi kitundu, sihitaji kuendelea kuwa dalali wa mafanikio ya kisiasa kwa ajili ya watu wa kaskazini dhidi ya watanzania wenzangu.

Nimejiuzuru uenyekiti wa mkoa wa SINGIDA kuanzia leo tarehe 3.11.2013 na kuahidi kuwa nitapambana mpaka mwisho wa tone la damu ya uhai wangu kuhakikisha demokrasia ya ndani ya chama hiki inaheshimiwa na kwamba watanzania hawadanganywi tena.

Nawashukuru sana.

Wilfred Noel Kitundu
Mwenyekiti Mkoa SINGIDA
Muasisi na mlezi wa CHADEMA Singida 1992-2013
Mjumbe wa Baraza Kuu TAIFA 1992 – 2013
Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa 1992-2013

1 comment:

  1. huo ni upepo mdogo sana!hauna impcts kabisa!alivuliwa uanachama hamad rashidi na kafulila!zaidi ndo wamejipotezea umaarufu tu!wakati hawa wachache wanaojiudhuru lakini tunasikia watu mashuhuri na wenye mvuto kwa jamii kuliko hata hao wanaojiudhuru,ila inakua wanajiunga na chama!tuone kama chama hakitapata mwenyekiti hapo singida!mimi mwenyewe nautaka sana huo uenyekiti nadhani ni wakati wangu kujisogeza hapo singida!

    ReplyDelete