Kijana Salum Nyangumwe (17) mshindi wa pili aliyeimba wimbo wa My Number One wa Msanii Nasib Abdul a.k.a Diamond wakati wa fainali za kusaka kipaji cha SUPA STAA wa watoto na vijana! la ”MO Kids Got Talent 2013" lililofanyika mwishoni mwa Juma kwenye Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi wetu.
Mtoto Moureen Julius(12), amejinyakulia kitita cha shilingi Milioni tano katika fainali za Shindano la “MO KIDS GOT TALENT 2013” lililofanyika kwenye hoteli ya Ledger Plaza Bahari beach lililoanza tarehe 25 hadi tarehe 28 mwezi huu ambapo fainali zilifanyika.
Shindano hilo lilijumuisha watoto zaidi ya mia mbili ambapo kila mmoja alijipatia nafasi ya kuonesha kipaji chake vikiwemo kuogelea, kuimba, kucheza, karate na vingine vingi.
Watoto 15 walichuana katika nusu fainali na kuchujwa hadi kufikia watoto watano na mwisho wa siku kupatikana SUPA STAA Moureen Julius aliyewafunika wenzake kwa kipaji alichonacho.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa mshindi wa kwanza aliyejinyakulia kitita cha sh.millioni tano, Mtoto Moureen Julius alisema pesa hizo alizoshinda atazitumia kwa kulipia ada na vifaa vingine vya shule.
Shindano hili la "MO KIDS GOT TALENT 2013" liliandaliwa na Frost Africa na kudhaminiwa na Mohammed Enterprises Tanzania Ltd. (MeTL) Group.
Supa Staa wa Shindano la "MO Kids Got Talent 2013" Moureen Julius (12) akionyesha kipaji chake cha kucheza kwenye fainali za shindano hilo.
Pichani juu na chini washiriki wa shindano la "MO Kids Got Talent 2013" wakiendelea kuonyesha vipaji vyao wakati wa fainali za shindano hilo.
Mtoto mwenye kipaji cha kuimba na kucheza.
No comments:
Post a Comment