December 13, 2013

LOWASSA ANUSURIKA KIFO AJALI YA NDEGE YA PRECISION ARUSHA LEO

Waziri Mkuu mtstaafu ambaye pia niMbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa ni mionghoni mwa abiria 37 na wafanyakzi 4  wa ndege ya Shirika la Ndege la Precion Air walionusurika kifo hii leo jijini Arusha.

Kiongozi huyo na wenzake walikjuwa wakisafiria ndege ya Precision Air aina ya ATR 42-600 na kupasuka magurudumu  manne ya nyuma wakati ikitua uwanja wa KIA jijini Arusha.

Lowassa alikuwa ni miongoni mwa abiria 37 na wahudumu 4 wa ndege hiyo iliyoruka salama majira ya saa 5:20 asubuhi ikitoka Dar es Salaam kwenda Arusha walionusurika kifo kufuatia ajali hiyo iliyotokea dakika chahe baada ya kutua katika uwanja wa Arusha leo.

Ndege PWI 422 iliyopata ajali imesababisha kuahirishwa kwa baadhi ya safari za shirika hilo la ndege leo ikiwepo ndege PW 430 iliyokuwa iruke Dar es Salaam leo saa 7:30 mchana kwenda arusha na kutua huko saa 10:55 jioni sasa itaruka saa 10 na kutua KIA saa 11:20 jioni.

Aidha taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air, Sauda Rajab imebainisha kuwa safari ya kwenda Zanzibar ya ndege PW 431 ikitokea Arusha nayo imesogezwa mbele.

Ndege ingine ambayo haita fanya safari zake kwa muda uliopangwa ni PW 431 iliyokuwa itoke Zanzibar kuja Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment