Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Angela Kizigha, akizungumza na
viongozi wa Jumuia hiyo katika Kata za wilaya ya Temeke, leo Mbagala,
kuwashukuru viongozi wa Jumuia ya Wazazi Kata zote za wilaya hiyo kwa
kumchagua kuwa Mwenyekiti katika uchaguzi uliopita. . Kushoto ni Katibu
wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Cholage.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Angela Kizigha, akimvalisha kitenge
cha sare maalum ya Jumuia hiyo, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kilakala,
Henedi Fereji, alipogawa sare hizo kwa wajumbe 60 waliohudhuria kikao
maalum kilichofanyika leo, Mbagala Kuu, kuwashukuru viongozi wa Jumuia
ya Wazazi Kata zote za Temeke, kwa kumchagua kuwa Mwenyekiti wa mkoa huo
katika uchaguzi uliopita. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi
Wilaya ya Temeke, Sophia Kinega na Watatu ni Katibu wa Jumuia hiyo mkoa
wa Dar es Salaam, Mohamed Cholage.
No comments:
Post a Comment