Baada ya kushuhudia
washindi kutoka mikoa mbalimbali nchini wakikabidhiwa zawadi zao zilizojumuisha
Pikipiki maarufu kama Boda boda pamoja na fedha taslim kutoka katika Promosheni
ya Timka na Boda Boda, Promosheni hiyo imeshuhudia kwa mara nyingine wakadhi wa
jiji la Dar es Salaam na sehemu zake nao
wakikabidhiwa Bodaboda hizo hafla iliyofanyika katika makao makuu ya ofisi za
kampuni ya Vodacom zilizoko Mlimani City.
Wakizungumza punde baada ya kukabidhiwa Pikipiki zao baadhi
ya washindi wamesema wamefurahi kuibuka wahindi katika Promosheni hiyo huku
wakitoa wito kwa Watanzania kuendelea kushiriki katika pomosheni hiyo ambayo
imebakiza siku chache kumalizika.
“Nimefurahi ana na kufarijika kuwa mshindi wa Promosheni
hiiya Timka na Boda Boda, Usafiri huu utanisaidia sana kutoka sehemu moja
kwenda nyingine watu wengi wanajua namna usafiri kwa jiji a dar ulivyo mgumu
lakini sasa nimepata suruhisho la tatizo hili nitakuwa nafika mahala pangu pa
kazi kwa urahisi na kuondoka bila matatizo na kwa gharama nafuu, alisema Mzee
Mustapha Bai, Moja ya washindi wa Pikipiki.
Kwa Upande wake Bwana, Steven Masawe ambaye ni Mwalimu wa
VETA Amesema “Nimeshiriki promosheni hii kwa hari sana nikijua ipi siku
nitashinda, na imekuwa kweli Pikipiki hii nitaipeleka kijijini kwetu migombani,
Kibosho Moshi, ikawasaidie katika usafiri kwani kutoka kijijini kwetu hadi
kufika mjini ni takribani kilomita 45 na usafiri ni wa tabu sana sasa kutokana
na kuwa mteja wa Vodacom nimewatatulia tatizo la usafiri.
Miongoni mwa washindi ambao walikuwa kivutio kwa watu
katika hafla hiyo ni ambaye ni mfanyakazi wa kazi za ndani Bi. Anastazia
Nyangige alipowaambia washindi wenzake kuwa ametumia mshahara wake kushinda
Bodaboda hiyo. “Mimi ni dada wa kazi za ndani sasa nitaendelea kufanya kazi
zangu na kumtafuta kijana ambaye ataiendesha Boda boda hii na kuniletea fedha
ili niweze kujiendeleza zaidi na ninaamini baada ya siku sitaweza tena
kuendelea kuwa dada wa kazi na nitakuwa mjasiriamali, alisema Nyagige.
Akizungumzia juu ya promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa
Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu amesema mpaka sasa kampuni yetu imekwishatoa
bodaboda 230 huku 200 bado hazijatolewa
mbali na hapo kuna kiasi cha shilingi milioni 142 tayari zimechukuliwa na
milioni 178 zimebakia.
“Promosheni hii imekuwa yenye mafanikio makubwa sana
kwani wateja wetu wameonesha mwitikio wa hali ya juu, promosheni hii inamlenga
kila mtu kwani tatizo la usafiri ni letu sote na pia kilio cha watu kutokuwa na
fedha za kukuza au kuongeza mitaji yao ya kibiashara ni kwa kila mtu. Kampuni
yetu ni sikivu siku zote, tunawajali na kuwasikiliza wateja wetu na ndio maana
tunawapatia kile wanachohitaji.” Aliongezea Nkurlu
Nkurlu aliongezea pia tunakabidhi bodaboda hizi kama
sehemu ya sikukuu za Krisimas na mwaka mpya na huku tukiwaahidi kuja na huduma
na ofa kemkem kwa ajili ya wateja wetu kwa mwaka ujao.
“Nawaasa washindi watakaopokea bodaboda hizi leo
kuzitumia ipasavyo kwa usafiri au kuwekeza katika biashara na kuleta manufaa
katika maisha yao. Pia ambao mpaka sasa hamjajiunga na promosheni hii, wakati
ni huu kwani Januari mwakani zoezi hili litakamilika na nitasikitika kuona kwa
nini hamshiriki kujishindia zawadi hizi.” Alimalizia Meneja huyo
Ili kujiunga na promosheni ya Timka na bodaboda wateja
wote wa Vodacom wanatakiwa kuandika neno PROMO na kutuma kwenda nambari 15544.
No comments:
Post a Comment