May 07, 2013

TANZANIA KUUNGANA NA KENYA NUSU FAINALI



Mei  mosi, jumatano iliyopita kupitia televisheni za  ITV na Clouds TV  katika kipindi cha 7 cha GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE tuliona timu ya Tanzania,Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad ikifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali pamoja na timu ya Kenya, Kenneth Kumau na Wills Ogutu, kutoka Nairobi ambao ndio walizishinda timu zote katika sehemu hii ya saba.

Wakenya walifanikiwa kupita katika hatua zote lakini wakapata ushindani kutoka kwa Waghana katika hatua ya Bullyese. Ilikuwa ni hatua ngumu lakini Wakenya ndio waliofanikiwa kufikia hatua ya pesa ukutani ambapo walifanikiwa kujishindia dola za kimarekani 1,500.

Daniel, Mwalimu, Kenneth na Wills wataendelea kuziwakilisha nchi zao kuwania kitita cha dola za kimarekani 250,000 na nafasi ya kuvishwa taji la ubingwa  wa Pan-African. Timu hizi mbili zitatakiwa kujiandaa vizuri zaidi na kujiamini ili ziweze kujinyakulia ushindi.

 Meneja wa kinywaji cha Guinness,Devis Kambi alisema, “Hongera kwa Daniel na Mwalimu kwa kufanikiwa kufuzu kuingia nusu fainali. Bado tunaendelea kuburudika na mashindano ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE baada ya kuona robo fainali wiki iliyopita. Sasa ushindani utakuwa mkali zaidi kwa kuwa tumebakiwa na timu nane tu katika nusu fainali. Timu zote sasa zinahitaji maandalizi ya kutosha ili ziweze kufanya vizuri katika hatua hizi za mwisho za kuelekea fainali. Kila la heri kwa timu zinazofuata kucheza wiki hii!”

Timu zitakazo shiriki katika robo fainali ya tatu ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE      :   

Kutoka Kenya watakuwa ni Enpantus Nyambura(24) na Samuel Papa(23) kutoka Nairobi, watavaa jezi nyekundu. Wakitarajia kufanya vyema zaidi kuliko awali Enphatus atakuwa kichwa cha timu wakati Samuel ataonesha kipaji chake cha kusakata kabumbu.
Watakaovaa jezi za bluu watakuwa ni wanafunzi wa Ghana, George Duah (21) na Yahya Issaka(20) kutoka Takoradi. George ni kichwa cha timu wakati Yahya ndiye atakayechezea mpira.Walifanikiwa kufuzu kuingia katika fainali ya kitaifa baada ya kujishindia  dola 3,000.
Kutoka Cameroon Florent Tonya(29) na Christian Lolo Mboko(24) kutoka Douala watavaa jezi za kijani katika robo fainali ijayo na katika hatua ya kitaifa wajishindia dola 3,000. Florent atajibu maswali wakati Christian atakuwa akionyesha kipaji chake cha kucheza soka.
Ghana itawakilishwa na Jonathan Naab(25) kutoka Tindogo na Desmond Odaano(26) kutoka Larteh watavaa jezi nyeusi katika robo fainali ijayo. Awali timu hii ilijishindia dola za kimarekani 5,500 katika hatua ya kitaifa. Jonathan atakuwa akipima maarifa yake wakati Desmond ataichezea mpira.

Robo fainali ya tatu ya Pan-African itarushwa katika televisheni za ITV na Clouds TV usikose kushuhudia timu kutoka Afrika Mashariki ikipambana vikali na nchi zingine za Afrika.
Wapenzi wa kipindi hiki cha Guiness football challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa karibu. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili  bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com kwa kupitia simu ya mkononi.  

Hakikisha kuufwatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali.
-www.facebook.com/guinnesstanzania

GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol.  Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku saa 3:15 ITV na saa 2:15 Clouds TV.

Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya Guiness wakati unaangalia kipindi hiki. 

Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa wale wenye umri chini ya miaka 18.

No comments:

Post a Comment