May 05, 2013

RAIS WA ZANZIBAR AWASILI PEMBA TAYARI KWA KUWASHA MWENGE WA UHURU


Rais wa  Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh, Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na baadhi ya viongozi wa jeshi na Usalama  wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Pemba, kwaajili ya uzinduzi  wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Chokocho wilaya ya Mkoani mkoa wa Kusini Pemba tarehe 6, Mei,2013.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mwanajuma Majid Abdalla katika kiwanja cha ndege  cha tayari kwa uzinduzi wa  mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa hapoMei 6,2013 katika  sheiha ya Chokocho, wilaya ya Mkoani mkoa wa Kusini Pemba.


Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mh,Balozi Seif Iddi (kulia) akisalimiana  na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh, Dkt. Fenella Mukangara (kushoto)  katika uwanja wa ndege Pemba,  alipowasili kwaajili ya kuhudhuria uzinduzi wa mbio  za Mwenge  wa uhuru Kitaifa Mei,6,2013 katika  sheiha ya Chokocho wilaya ya Mkoani mkoa wa Kusini Pemba.

Baadhi wa viongozi wa chama na serikali wakiwa katika uwanja wa ndege wa Pemba kumlaki Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  Mh. Dkt.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani), kwaajili ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Chokocho Wilaya ya Mkoani, mkoa wa Kusini Pemba, Mei 5,2013.


Kikundi cha brass- band ya vijana  wakitumbuiza wakati wa mapokezi ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mh. Dkt. Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) katika uwanja wa ndege wa Pemba ,Mei,5,2013. Picha : Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.

No comments:

Post a Comment